Tuesday, October 11, 2016

Machupa aipandisha daraja FC Kilimanjaro kwenye ligi nchini Sweden

Timu inayomilikiwa na watanzania nchini Sweden, FC Kilimanjaro imefanikiwa kupanda daraja kwenye moja ya ligi iliyokuwa ikishiriki nchini humo.unnamed-19Timu hiyo imepiga hatua hadi kufikia kucheza ligi daraja la sita kwa sasa ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi April, mwakani. FC Kilimanjaro imefanikiwa kupanda daraja ikiwa na jumla ya pointi 41 huku ikifuatiwa na timu waliyocheza nayo kwenye mchezo wao wa mwisho Solna FC ambao walifungana bao 1-1 iliyokuwa na pointi 40.Goli la FC Kilimanjaro lilifanikiwa kufungwa na mchezaji wa zamani wa Simba, Athuman Machupa. Timu hiyo ina mchanganyiko ya wachezaji kutoka sehemu mbalimbali akiwemo golikipa Lamin Jowo (Gambia), Mike Obi Otieno (Kenya), Mohammed Pato (Somalia) na Ahmad Zohib (Morocco).unnamed-16Akiongea na Bongo5, kocha mkuu wa timu hiyo Humphrey James amesema, “Pasipo shaka kutokana na mikakati pamoja na mipango tuliyojiwekea bila shaka tutayafikia malengo yetu ya kucheza ligi za juu. Unajua mtu akiangalia namba anajua safari ni ndefu sana ila si hivyo kama tukifanikiwa kupanda kila mwaka kwa kipindi cha miaka minne ina maana tutakuwa katika mfumo wa kulipwa.”Kocha huyo ameongeza kuwa muda uliopo ni mchache sana wanatakiwa kujipanga zaidi ili kuweza kufikia malengo yao.unnamed-20

No comments:

Post a Comment