Showing posts with label Michezo kitaifa. Show all posts
Showing posts with label Michezo kitaifa. Show all posts

Wednesday, October 12, 2016

VPL: Yanga levo kubwa, Simba vinara, Stand united ushindi

VINARA wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Simba Leo wameendelea kujichimbia kileleni baada ya kuifunga Mbeya City wakati Mabingwa Watetezi Yanga wakijikusanya kwa ushindi toka kwa Mtibwa Sugar huku Azam FC wakizidi kudidimia baada ya kufungwa na Stand United iliyojizatiti kushangaza na kuwania Ubingwa.
VPL: LIGI KUU VODACOMMatokeo:Jumatano Oktoba 12Mbeya City 0 Simba 2Mwadui FC 2 African Lyon 0Mbao FC 3 Toto Africans 1Maji Maji FC 0 Kagera Sugar 1Stand United 1 Azam FC 0JKT Ruvu 0 Tanzania Prisons 0Yanga 3 Mtibwa Sugar 1
Jijini Dar es Salaam, Uwanja wa Uhuru, Yanga, waliitwanga Mtibwa Sugar Bao 3-1 walipoongoza 1-0 hadi Haftaimu kwa Bao la Mzambia Obrey Chirwa akifunga Bao lake la kwanza kwenye Ligi ambalo alipachika Dakika 1 kabla Haftaimu.Kipindi cha Pili Mtibwa Sugar walisawazisha Dakika ya 63 kupitia Harun Chanongo lakini Simon Msuva akaipa Yanga Bao la Pili Dakika ya 68 na Mzimbabwe Donald Ngoma, aliengizwa kuchukua nafasi ya Obrey Chirwa aliipa Yanga Bao la 3.Huko Sokoine, Mbeya, Bao za Kipindi cha Kwanza za Ibrahim Ajib na Shiza Kichuya ziliipa Simba ushindi wa 2-0.Nao Azam FC, Timu inayofifia vibaya Msimu huu, ilitunguliwa 1-0 na Stand United, Timu inayokuja juu mno na imo kwenye mbio za Ubingwa, kwenye Mechi iliyochezwa huko Kambarage, Shinyanga.Matokeo haya yamewachimbia Simba kileleni wakiwa na Pointi 20 kwa Mechi 8, wakifuata Stand United wenye Pointi 19 kwa Mechi 9, kisha Kagera Sugar wana Pointi 15 kwa Mechi 9 na Yanga wako Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 14 kwa Mechi 7.Mtibwa Sugar ni wa 5 wakiwa na Pointi14 kwa Mechi 9.----------------------------------------------VPLYANGA - Mechi zao:Okt 16 Yanga v Azam FCOkt 19 Toto African v YangaOkt 22 Kagera Sugar v YangaOkt 26 Yanga v JKT RuvuOkt 29 Yanga v Mbao FCSIMBA - Mechi zao:Okt 15 Simba v Kagera SugarOkt 20 Simba v Mbao FCOkt 23 Simba v Toto AfricanOkt 29 Mwadui v SimbaNov 2 Stand United v Simba----------------------------------------VPL: LIGI KUU VODACOMRatiba:Alhamisi Oktoba 13Ruvu Shooting v Ndanda FC.


Chanzo:Sokaintanzania

Tuesday, October 11, 2016

Yanga Vs Mtibwa kesho uwanja wa Uhuru

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano Oktoba 12, 2016 kwa michezo saba huku ule mchezo kati ya Yanga ya Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro ukipangwa kufanyika Uwanja wa Uhuru jijini.Kwa mujibu wa Kanuni ya 6 kipendelea cha kwanza, Yanga wametambulisha Uwanja wa Uhuru kama uwanja wa nyumbani kwa sasa baada ya kupeleka maombi Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF) ambako baada ya kuyafanyiwa tathimini kwa mujibu kanuni hiyo ya sita, kipengele cha sita, TFF imeiridhia klabu hiyo ya Mtaa wa Jangwani, kutumia uwanja wa Uhuru.

Hatua hiyo inafuatia na Serikali ambaye ndiye mmiliki wa viwanja vya Uhuru na Uwanja Mkuu wa Taifa, kuzuia klabu hiyo pamoja na ya Simba kutumia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa michezo yao ya nyumbani kutokana na vurugu.
Michezo mingine itakayopigwa Jumatano ni kati ya Mbeya City ya Mbeya na Simba ya Dar es Salaam, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya; Majimaji itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.
Stand United itaikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga na katika mkoa huo huo Mwadui itakuwa mwenyeji wa African Lyon kwenye dimba la Mwadui Complex huku timu pinzani za Mwanza ‘Mwanza Derby’ kati ya Mbao na Toto Africans itapigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo. Alhamisi Oktoba 13, 2016 Ruvu Shooting itacheza na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Mabatini.

TFF yaingilia sakata la Yanga kuikodishwa yamtaka katibu Mkuu aonyeshe mkataba

Baada ya taarifa za Yanga kuingia mkataba wa kuikodisha timu kwa miaka kumi kwa Kampuni ya Yanga Yetu zimezidi kuchukua sura mpya ambapo licha ya baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kupinga utaratibu uliotumika, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) nalo limefunguka kuhusu jambo hilo.Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amezungumza kuhusu mabadiliko ambayo wameyafanya na kusema wao kama TFF bado hawajayatambua mabadiliko hayo na wamemwandikia barua Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit ya kumtaka aonyesha mkataba ambao wameingia na kampuni ya Yanga Yetu.“Nimemuandika barua Katibu Mkuu wa Yanga atupe nakala ya mkataba ule (wa Yanga na Kampuni ya Yanga Yetu), ili kama kuna wasiwasi hilo tatizo lishughulikiwe mapema maana hizi klabu niza wanachama, wanaweza kuingia mikataba na wanachama wengine wakaja na mambo mengine,“Tunataka mkataba uwe wazi ili hata klabu zingine zijifunze, kwahiyo Yanga tumewaomba walete copy ya huo mkataba nini kinaazimwa na kipi kinauzwa, klabu itaendeshwaje na baada ya hapo kamati za TFF zitakaa kulijadili jambo hilo, kama itakuwa tofauti na kanuni zetu tutarudi kwao warekebishe mambo ambayo hayapo sawa,” alisema Mwesigwa na kuongeza.“Uendeshwaji lazima ubadilike kuendana na wakati lakini hatutaki mabadiliko yasababishe mvurugano ambao haukuwepo kwa muda mrefu na tumeshapokea barua nyingi za wanachama wa Yanga hadi wazee wamekuja wanasema wanataka kwenda kumwona mkuu wa nchi”Aidha alisema TFF bado inatambua Yanga inasimamiwa na uongozi wa klabu kama ilivyokuwa awali ikiongozwa na Mwenyekiti, Yusuph Manji na kama kutakuwa na jambo la tofauti watatoa taarifa baada ya kujiridhisha mfumo ambao Yanga itakuwa inautumia kukodisha timu kwa Kampuni ya Yanga Yetu.


Source: Dewjiblog.

Machupa aipandisha daraja FC Kilimanjaro kwenye ligi nchini Sweden

Timu inayomilikiwa na watanzania nchini Sweden, FC Kilimanjaro imefanikiwa kupanda daraja kwenye moja ya ligi iliyokuwa ikishiriki nchini humo.unnamed-19Timu hiyo imepiga hatua hadi kufikia kucheza ligi daraja la sita kwa sasa ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi April, mwakani. FC Kilimanjaro imefanikiwa kupanda daraja ikiwa na jumla ya pointi 41 huku ikifuatiwa na timu waliyocheza nayo kwenye mchezo wao wa mwisho Solna FC ambao walifungana bao 1-1 iliyokuwa na pointi 40.Goli la FC Kilimanjaro lilifanikiwa kufungwa na mchezaji wa zamani wa Simba, Athuman Machupa. Timu hiyo ina mchanganyiko ya wachezaji kutoka sehemu mbalimbali akiwemo golikipa Lamin Jowo (Gambia), Mike Obi Otieno (Kenya), Mohammed Pato (Somalia) na Ahmad Zohib (Morocco).unnamed-16Akiongea na Bongo5, kocha mkuu wa timu hiyo Humphrey James amesema, “Pasipo shaka kutokana na mikakati pamoja na mipango tuliyojiwekea bila shaka tutayafikia malengo yetu ya kucheza ligi za juu. Unajua mtu akiangalia namba anajua safari ni ndefu sana ila si hivyo kama tukifanikiwa kupanda kila mwaka kwa kipindi cha miaka minne ina maana tutakuwa katika mfumo wa kulipwa.”Kocha huyo ameongeza kuwa muda uliopo ni mchache sana wanatakiwa kujipanga zaidi ili kuweza kufikia malengo yao.unnamed-20

Monday, October 10, 2016

Yanga waridhia kutumia uwanja wa Uhuru, kukipiga na Mtibwa Oktoba 12

Uwanja wa Uhuru mpya
Keshokutwa Jumatano Oktoba 12, 2016 Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kwa michezo saba huku ule mchezo kati ya Young Africans ya Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro ukipangwa kufanyika Uwanja wa Uhuru jijini.Kwa mujibu wa Kanuni ya 6 kipendelea cha kwanza, Young Africans wametambulisha Uwanja wa Uhuru kama uwanja wa nyumbani kwa sasa baada ya kuleta maombi Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF) ambako baada ya kuyafanyia tathimini kwa mujibu kanuni hiyo ya sita, kipendelea cha sita, TFF imeiridhia klabu hiyo ya Mtaa wa Jangwani, kutumia uwanja wa Uhuru.Hatua hiyo inafuatia na Serikali – mmiliki wa viwanja vya Uhuru na Uwanja Mkuu wa Taifa, kuzuia klabu hiyo pamoja na ya Simba kutumia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa michezo yao ya nyumbani kutokana na vurugu.Michezo mingine itakayopigwa Jumatano ni kati ya Mbeya City ya Mbeya na Simba ya Dar es Salaam, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya; Majimaji itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.Stand United itaikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga na katika mkoa huo huo Mwadui itakuwa mwenyeji wa African Lyon kwenye dimba la Mwadui Complex huku timu pinzani za Mwanza ‘Mwanza Derby’ kati ya Mbao na Toto Africans itapigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo. Alhamisi Oktoba 13, 2016 Ruvu Shooting itacheza na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Mabatini.

Sunday, October 9, 2016

Kwenye VPL Vigogo wanarejea dimbani wiki hii

VPL-OKT9

VPL, Ligi Kuu Vodacom, itaendelea Jumatano hii na kuwahusisha Vigogo Mabingwa Watetezi Yanga, Vinara wa sasa Simba na Azam FC baada ya kutohusishwa kwa Mechi za Wikiendi hii kutokana na Mechi za Kimataifa.
Jana Timu ya Taifa ya Tanzania ilipangiwa kucheza Mechi ya Kirafiki na Ethiopia huko Addis Ababa lakini Mechi hiyo kufutwa kutokana na sababu za kiusalama za huko Ethiopia.
Jumamosi zilchezwa Mechi 3 za VPL.na Timu ya mkiani Majimaji FC kuambua Pointi 3 za kwanza Msimu huu lakini bado wapo mkiani baada ya kuifunga Mbao FC 1-0.
Mechi nyingine za Juzi zilikuwa Sare ya 0-0 kati ya Ruvu Stars na Mtibwa Sugar na African Lyon kuifunga 1-0 Ndanda FC.
Jumatano Wiki hii zipo Mechi 7 za VPL na Mabingwa Yanga wapo Nyumbani kucheza na Mtibwa Sugar wakati Vinara Simba wapo Ugenini huko Sokoine kuivaa Mbeya City.
Azam FC watakuwa huko Kambarage Shinyanga kucheza na Stand United.
VPL: LIGI KUU VODACOM
Ratiba
Jumatano Oktoba 12
Mbeya City v Simba 
Mwadui FC v African Lyon 
Mbao FC v Toto Africans 
Maji Maji FC v Kagera Sugar 
Yanga v Mtibwa Sugar 
Stand United v Azam FC 
JKT Ruvu v Tanzania Prisons.

Tambwe ana haya kwa washambuliaji wa vikosi mbali mbali 255

Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe amesema siri ya kuendelea kutikisa nyavu katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara bila kushuka, ni kwa vile amekuwa hasikilizi maneno ya mashabiki uwanjani.

Alisema mchezaji yeyote kama anahitaji kufanikiwa na kufanya vizuri katika ligi hiyo hapa nchini hana budi kuziba masikio ya mashabiki na kufanya kile ambacho kimemleta katika timu vinginevyo ni rahisi kupotea.

Tambwe hivi karibuni aliifungia bao timu yake katika mchezo dhidi ya Simba, ingawa inadaiwa kabla ya kufunga aliushika kwa mkono mpira huo.

mchezaji huyo wa zamani wa Simba, alisema anawajua mashabiki wengi wa soka wamekuwa ni wazungumzaji, na kwamba kama angekuwa anawafuatisha angekuwa ameshuka kiwango.

“Siku zote ukitaka kufanikiwa katika Ligi ya Tanzania ni lazima upambane kweli na kuacha kusikiliza maneno ya mashabiki, kwani ukiwafuatisha utaanguka na kupotea kabisa,” alisema.

Tambwe tangu kujiunga na Simba msimu wa mwaka 2013 na msimu uliopita Yanga, amekuwa akizidi kuonesha ubora wake katika kufumania nyavu huku msimu uliopita akiibuka kuwa mfungaji bora.

Saturday, October 8, 2016

CAF kutua Tanzania, wanakuja kwaajili ya ukaguzi

caf
Upande wa soka yeto Bongo, Wataalamu wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), wanatarajiwa kutua nchini wakati wowote kuanzia sasa kwa ajili ya kukagua Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Huu ni utaratibu wa CAF ambako baada ya muda hutembelea nchi wanachama kuangalia maendeleo ya miundombinu ya mpira wa miguu kabla ya kupandisha hadhi ya viwanja kwa ajili ya michuano ya kimataifa inayosimamiwa na kuendeshwa na CECAFA, CAF na FIFA.
Ukaguzi huo unafanyika wakati Tanzania inasubiri majibu ya Uwanja wa Sokoine wa Mbeya ambao ulikwiisha kukaguliwa na mapendekezo ya uboreshwaji kutolewa ili uweze kupandishwa hadhi ya matumizi ya kuchezwa mechi kubwa kama vile fainali za Kombe la Shirikisho, Ngao ya Hisani, michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na mechi kubwa za kimataifa za kirafiki na mashindano ya CECAFA, CAF na FIFA.
Viwanja ambavyo CAF na FIFA inavitambua nchini Tanzania hadi sasa ni Amani wa Unguja, Zanzibar; Kaitaba wa Kagera, Azam Complex na Uwanja Mkuu wa Taifa vya Dar es Salaam.
Endapo CCM Kirumba utapitishwa, kutakuwa na nafasi ya kuruhusu kuchezwa mechi kubwa kama vile fainali za Kombe la Shirikisho, Ngao ya Hisani pamoja na mechi kubwa za kimataifa za kirafiki na mashindano ya CECAFA, CAF na FIFA.
Kirumba inaingia kwenye orodha ya viwanja vya Gombani ulioko Pemba; Sokoine wa Mbeya, Kaitaba wa Kagera ambavyo vilikwisha kukaguliwa na sasa vinasubiri kupitishwa ili kutumika kimataifa. Ujio wa viwanja hivyo, utapanua wigo wa Tanzania kuandaa michuano mikubwa katika ngazi ya timu za taifa kimataifa.

Taarifa za kukodishwa kwa Yanga zina ufafanuzi wake hapa!

Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) imesema kuwa mkataba wa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kukodishwa klabu hiyo ni batili. Tamko hilo limetolewa jana oktoba 7 na Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Mohamed Kiganja baada ya juzi kusambaa kwa taarifa ya mkataba wa Yanga katika mitandao ya kijamii.
Suala la Yanga kukodishwa timu lilianza mchakato tangu Manji aitishe mkutano mkuu wa dharura miezi miwili iliyopita, akiomba ridhaa ya wanachama wa klabu hiyo kumkodisha timu na nembo kwa miaka 10, ombi ambalo lilipitishwa na kurudishwa katika bodi ya wadhamini kwa ajili ya kufanyiwa kazi na juzi kupitishwa kwa makubaliano hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kiganja alisema wanaunga mkono suala la mabadiliko, lakini lazima yafuate sheria na taratibu zilizowekwa ili kukamilisha mabadiliko yoyote.
“Mimi sipingi klabu zetu kufanya mabadiliko isipokuwa najaribu kukumbusha zifuate utaratibu wa kisheria, kwa sababu unapobadilisha jina au kufanya marekebisho yoyote ni lazima vikasajiliwe na kutambulika,”alisema.
Kiganja alisema hata Bodi ya Yanga iliyohusika kuruhusu timu hiyo kukodishwa haitambuliki kwa Msajili, kwa vile wajumbe wake wengi ni wale waliochaguliwa kwa mpito. Alisema bodi ya wadhamini iliyoundwa Julai 5, 1973 ni wawili tu wanaotambulika waliopo hadi sasa ambao ni Jabir Katundu na Juma Mwambelo.
Lakini, Mwembelo amekuwa ahusishwi tena katika mambo yanayoendelea ya timu hiyo. Bodi ya mpito, ambayo Kiganja alisema hawakusajiliwa wala kupitishwa kwenye mkutano mkuu kutokana na taratibu ni George Mkuchika, Fatuma Karume, Francis Kifukwe, Amri Ramadhan, Juma Kambi na Abeid Mohamed.
Katibu huyo alifafanua taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili timu ikodishwe kuwa ni kutumia vikao, ambapo cha kwanza ikiwa ni Kamati ya Utendaji ya Klabu itakayochambua hoja na kukubaliana au kutokukubaliana kisha kupeleka katika kikao cha ngazi za juu.
Pia, alisema baadaye hoja inapelekwa kwenye mkutano mkuu wa wanachama wote uwe wa dharura au kawaida ili kujadiliana hoja husika, kisha baada ya kukubaliana au kutokukubaliana inapelekwa kwa Baraza la wadhamini lenye uwezo wa kuingia kwenye maamuzi makubwa, na mwisho inapelekwa kwa msajili.
“Kwa mujibu wa sheria ya BMT ya mwaka 1967 kifungu namba 11 (1) kinaeleza chama chochote kinachofanya mabadiliko ya jina, anuani, madhumuni au kifungu chochote cha Katiba yake kitatakiwa kipate idhini ya msajili,”alisema.
Alisema kifungu namba 11 (3) msajili anaweza kuyakataa maombi ya kubadili kifungu chochote cha katiba kama ataona kuwa mabadiliko yanaweza kuhatarisha usalama na kuvuruga amani, au kama kuna malengo ya kuwanufaisha wachache au kama hayazingatii sera za michezo na sheria za BMT.
Alisema baada ya hatua hizo kukamilika, inabidi kufanya marekebisho ya Katiba ambayo yatapitia kwenye taratibu za klabu, na ndipo klabu husika itakuwa imepata baraka za serikali.
Katibu huyo aliweka wazi kuwa amezungumza hayo kwa kuwa yeye ni kiongozi na mlezi wa vyama vya michezo nchini na kwamba, maelezo yake hayalengi kuwakatisha tamaa wale walionesha nia ya kuwekeza kwenye michezo bali kuwambushana mambo ya msingi kwa manufaa.

Thursday, July 28, 2016

Video: Genk anayochezea Samatta alivyoibuka ushindi Julai 28, 2016


KRC Genk wamekutana na Cork City, baada ya kuitoa Buducnost ya Montenegro kwa mikwaju ya penati 4-2, baada ya mechi yao ya mwisho kumalizika kwa Buducnost kuibuka na ushindi wa goli 2-0 ila kutokana na kuwa na aggregate ya 2-2 walilazimika kucheza dakika 120 na baadae mchezo ukaamuliwa kwa mikwaju ya penati.
licha ya KRC Genk kupata ushindi huo wakiwa pamoja na nyota wao kutokaTanzania Mbwana Samatta, bado wana wakati mgumu katika mchezo wa marudiano watakaocheza August 4 Ireland, kwani watakuwa wanahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ile ili waweze kusonga mbele katika hatua inayofuata na kuitoa Cork City.

Wednesday, July 27, 2016

Tp Mazembe Waipa waitumainisha Yanga kufusu fainali ya CAF


Maombi na furaha ya watanzania wote wazalendo ni kuona Yanga ikifanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika CAF, licha ya kuwa nafasi yao kwa sasa inatajwa kuwa ndogo, lakini Yanga wanayo nafasi ya kusonga mbele licha ya kuwa na point moja na wapo mkiani.
Safari ya Yanga kutinga hatua ya nusu fainali ya CAF inamlazimu ashinde mechi zake zote mbili zilizosalia za MO Bejaia atakayocheza nyumbani na mechi dhidi ya TP Mazembe atakayocheza ugenini, huku akiombea mechi ya mwisho kati ya MO Bejaia yaAlgeria dhidi ya Medeama imalizike kwa sare ya aina yoyote ile.
TP Mazembe bado imeendelea kuipa matumaini Yanga baada ya mchezo wa leo kufanikiwa kuifunga MO Bejaia kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Rainford Kalabadakika ya 62, kwani kama TP Mazembe angefungwa leo Yanga wangekuwa rasmi wameaga michuano hiyo wakiwa wamesalia na michezo yao miwili mkononi.

Tuesday, July 26, 2016

Hatimaye Yanga nusu fainali ya CAF yanyong'onyezwa

Leo ilikuwa ni siku nyingine kwa wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika, klabu ya Dar es Salaam Young Africans kucheza mchezo wake wa nne wa Kundi A Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Medeama yaGhana.
Yanga wamecheza mchezo wao wa nne dhidi ya Medeama mjini Takoradi Ghana na kukubali kipigo cha goli 3-1, kipigo ambacho kimezidi kufifisha safari ya Yanga kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo, magoli ya Medeama yamefugwa na Daniel Amoah dakika ya 7 na Abbas Mohammed aliyefunga magoli mawili dakika ya 22 na 37.
Simon Msuva ndio aliyefunga goli la kufutia machozi kwa Yanga kwa mkwaju wa penati dakika ya 24, kwa matokeo hayo Yanga wanaendelea kusalia na michezo miwili dhidi yaMO Bejaia ya Algeria watakaocheza nyumbani na TP Mazembe ya Kongowatakaocheza ugenini, nafasi ya Yanga kufuzu katika hatua ya nusu fainali ni finyu sana.

Mkwasa ameita wachezaji 24 Taifa Stars....wawili wakubwa hawapo!

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa leo July 26 2016 ametangaza kikosi cha wachezaji watakaoanza maandalizi ya kucheza mchezo wa kukamilisha ratiba wa michuano ya AFCON dhidi ya Nigeria, Mkwasa ameita kikosi hicho baada ya ombi lao la mchezo wao dhidi ya Nigeria kufutwa kukataliwa.
Wachezaji hao walioitwa na Mkwasa wanatakiwa kuripoti kambini July 31 2016 na kuanza kambi ya siku tano itakayomalizika August 5 2016, hata hivyo kuelekea mchezo huo waNigeria utakaochezwa mwanzoni mwa mwezi September utawakosa wachezaji wanaocheza soka nje ya nchi kama Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Magolikipa
Deogratus Munish, Beno Kakolanya (Yanga), Aishi Manula (Azam FC) Mabeki
Oscar Joshua,  Kelvin Yondani, Juma Abdul (Yanga), Erasto Nyoni, Agrey Morris (Azam FC) Mohamed Hussein (Simba ).

Viungo
Farid Musa, Himid Mao (Azam FC), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude (Simba), Ibrahim Rajab ‘Jeba’ (Mtibwa Sugar ), Hassan Kabunda (Mwadui FC), Simon Msuva, Juma Mahadh (Yanga ).

Washambuliaji
Joseph Mahundi (Mbeya City), Ibrahim Ajib, Jamal Mnyate (Simba), John Bocco (Azam FC) na Jeremiah Juma (Tanzania Prisons).

Sunday, July 24, 2016

CHUNGU, TAMU MIEZI 32 YA MALINZI TFF


ZIMEBAKI siku 98,  Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, atimize miaka mitatu tangu aiingie madarakani usiku wa kuamkia Oktoba 28, 2013 kuliongoza shirikisho hilo lenye mamlaka ya juu kisoka nchini.
Kuna mambo mengi yanayohusu soka la Tanzania yaliyofanyika katika kipindi hiki cha miezi 32 na siku 27 cha uongozi wa Malinzi, lakini sehemu kubwa ya mipango na uamuzi uliofanya na utawala wa rais huyo haukuwa na tija kwa maendeleo ya mchezo huo nchini tena huenda ukawa hauambatani na sera za utawala bora.
Makala haya yanaangalia baadhi ya mambo mabaya na mazuri yaliyofanywa na uongozi wa Malinzi tangu aingie madarakani kumrithi mtangulizi wake, Leodegar Tenga. Swali kubwa ambalo mdau wa soka nchini anaweza kujiuliza ni je Utawala bora kwa Malinzi uko wapi?
TFF YAMSHINDWA JERRY MURO
Mnamo Oktoba 19, 2011 kwenye mkutano wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) uliofanyika Zurich, Uswisi ukiongozwa na Mkurugenzi wa wanachama na maendeleo ya FIFA, Thierry Regenass, kamati ya utendaji na viongozi wa mashirikisho ya soka ulizokutanisha nchi wanachama. Lengo la mkutano ulikuwa ni wa FIFA kueleza marais wa mashirikisho kuwa wana mamlaka ya kusimamia soka kwa kuzingatia sheria lakini kwa nafasi ya kufanya chochote.
Rais wa TFF, Malinzi ni kama ameshindwa kutambua hilo haswa kwenye sakata linalomuhusu msemaji wa Yanga, Jerry Muro ambaye hivi karibuni ameonekana kuwa na ubavu mkubwa zaidi ya shirikisho hilo.
Julai 7 mwaka huu, Kamati ya maadili ya TFF chini ya mwenyekiti wake, Wilson Ogunde ilimfungia Muro kujihusisha na mambo ya soka kwa mwaka mmoja na faini ya milioni tatu lakini msemaji huyo aliidindia TFF siku hiyo hiyo na kusema kuwa shirikisho hilo.
Inashangaza kuwa licha ya kuwa kuna zaidi ya wasemaji wa klabu 50, yaani wa timu za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL), Muro ndiyo msemaji pekee ambaye amekuwa akiishambulia TFF kwenye vyombo vya habari kwa kigezo kuwa hawawezi kumwambia kitu kwa kuwa TFF haijamuajiri.
Muro alipelekwa kwenye kamati ya maadili akituhumiwa kupingana na maamuzi pamoja na kuishambulia TFF kwenye vyombo vya habari.
Moja ya kauli ya muro kwa TFF baada ya kusimamishwa, “TFF haiwezi kuniambia niache kuzungumzia klabu yangu, TFF haijaniajiri na hainilipi mshahara. Mwajiri wangu ndiye anayeweza kuniambia nisizungumze kwasababu  hao ndiyo walioniweka pale wakijua mimi ni mtu makini.
AMUUNGA MKONO MTUHUMIWA WA ‘RUSHWA’
Desemba 2014, TFF chini ya Malinzi  iliweka msimamo wake kwa kumuunga mkono Sepp Blatter  kwenye uchaguzi wa Urais wa FIFA, Blatter alishinda lakini miezi kadhaa mbele ilibainika kuwa alikabiliwa na sakata kubwa la rushwa lililopelekea yeye kung’olewa kwenye nafasi yake.
Kwa hatua ya Malinzi kumuunga mkono Blatter, maswali mengi yalibaki miongoni mwa wadau ya Je Malinzi ni msafi? Je kama alikuwa akimpa sapoti Blatter, na rais huyo akangolewa kwa rushwa iwaje yeye awe msafi?
AWAWEKA NJIA PANDA STAND UNITED NA STAND UNITED COMPANY
TFF imelitolea maamuzi sakata la Stand United na lile kundi lililodai kuwa timu hiyo inatambulika kwa jina la Stand United Company lakini maamuzi ya TFF yamekuwa ni ya kusuasua kwa muda mrefu kwani walishindwa kufanya maamuzi ya hapo kwa hapo.
Matokeo ya kuchelewa yaliweka pande zote mbili njia panda, Stand United imekuwa ikifanya usajili kwa kususua bila ya kufahamu kama wanachokifanya ni sahihi.
Matokeo ya mgogoro huo ni timu hiyo kushindwa kusajili. Mnamo Julai 8, mwaka huu, Uongozi sahihi wa timu hiyo kupitia kwa msemaji wake, Deokaji Makomba alidai kuwa wameshindwa kusajili kwasababu ya kuvurugwa na kundi linalojiita Kampuni linaloongozwa na Mkurugenzi wao Dk Jonas Tiboroha.
Uchunguzi uliofanywa na Lete Raha umebaini kuwa akaunti ya Mfumo wa KIelektoniki wa Usajili yaani TMS ya klabu ya Stand imebadilishwa namba ya siri hivyo uongozi wa sasa wa timu hiyo umeshindwa kuingia kwenye mtandao huo kwa siku za karibuni.
Makomba alipoulizwa juu wa TMS kufungiwa alisema, “Tulikuwa tukiingia mara kwa mara kwenye akaunti yetu ya mfumo wa elekroniki ya usajili kwani tulikuwa na namba ya siri ya kufanya hivyo lakini ilivyoibuka mgogoro, inaonekana TFF walibadili namba ya siri.
“Tunashangazwa na hilo, kama TFF ilikuwa inatutambua ilikuwa inapaswa kuturuhusu sisi kuingia kwenye mtandao lakini hata nilipowasiliana na wahusika nimekuwa nikipigwa danadana, matokeo yake hata wale wanaojiita kampuni wamekuwa wakisajili licha ya kuwa TFF imedai haiwatambuhi,”alifafanua msemaji huyo.
Stand United halisi hivi karibuni ilimsajili mshambuliaji Adam Kingwande kutoka Kagera Sugar lakini siku mbili badaye wale wanaojiita Stand United Company walimpa mkataba mpya winga Haruna Chanongo ambaye Stand United halisi ilishatangaza kuachana naye.
Straika Paul Nonga ni moja ya wachezaji walioachwa njia panda na mgogoro huo huku mwenyewe akidai kuwa anachanganywa na mgogoro wa klabu hiyo na hivyo hawezi kusaini mpaka ple atakapoona mambo ni mazuri. Anasema, “ Nilifanya mazungumzo na Stand United halisi, pia Stand United Company ilinitafuta na tukazungumza lakini sielewi wapi sahihi. Mimi na rafiki zangu wengi tumekuwa tukikwama hivyo.”