Friday, May 27, 2016

New music Video: Bill Nass Feat Barnaba - Demu Gani ( Watch and Download free )


Karibu kwa mara nyingine kutizama video mpya ya Bill Nas ya wimbo wake unaokwenda kwa jina la Demu gani ambayo amemshirikisha Barnaba Classic.

Video hii haina taarifa rasmi kuhusu kuachiwa ila baada kupita huku na kule nimeweza kuibahatisha nikaona ni vema nikuletee uweze kuitizama kisha uache maoni yako.


Video imesimamiwa na kampuni ya LFLG na audio imefanywa na Mesen Selekta pale Defatality.

New music Video: Bill Nas - Chafu Pozi ( Official Video Watch and Download )


Karibu kutizama video mpya ya wimbo wa Bill Nas unaoitwa Chafu pozi ambao tayari audio yake imekamata nafasi za juu kwenye vituo mbali mbali vya redio.

Video imetayarishwa na kampuni ya  LFLG 

Itizame hapo chini na uache maoni yako.


Thursday, May 26, 2016

New music Video: Tox Star - Candle light ( Official Video Watch and Download )


Genious Geff ndo kaongoza video hii mpya ya Toxstar inayokwenda kwa jina la Candle light ambapo audio yake
ameifanya Bob Junior pale Sharobaro record.

Karibu kuitizama kisha uache maoni yako hapo chini.

DOWNLOAD MP4 HERE

Wednesday, May 25, 2016

New music Video: Real Jofu ft. Nay Wamitego - Unanionea ( Official Video Download )

New music Video: Mayunga feat Akon - Please Don't Go Away ( Official Video Download )

New music Video: G Nako Ft Chin Bees & Nikki Wa II - Arosto ( Official Music Video Download )

Tizama video mpya ya G Nako aliwashirikisha Chin Beez na Nikki wa pili inaitwa Arosto ambayo imeongozwa na
Hanscana na audio imefanywa na Lufa pale Switch Records.


New music Video: Kadjanito - One More Night ( Official Video Watch and Download )

New music Video: Alikiba - Aje ( Official Video Watch and Download )

Karibu kutizama video mpya ya msanii Alikiba inaitwa Aje ambayo amemshirikisha M.I. Video imeongozwa na phenomenal Director Meji chini ya uongozi
wa ROCKSTAR4000.

Karibu kuitizama na kudownload.



Kama bado Audio hukuwa nayo Download HAPA

Saturday, May 21, 2016

Wewe sio mwaminifu kwa mpenzi wako?, umejiuliza kwanini....!!!?


Hapa nazungumza na wale ambao wanatamani kuwa waaminifu kwa wapenzi wao. Yapo mambo mengi, lakini hapa ninajitahidi kueleza yale ya muhimu zaidi. Wiki iliyopita niliishia kwenye kipengele cha mitandao ya kijamii, kwa kuwa sikukimaliza, tutaendelea hapo.MITANDAO YA KIJAMII
Utafiti usio rasmi unaonesha kwamba, pamoja na kwamba mitandao ya kijamii imesaidia kwa kiasi kikubwa sana kurahisisha upatikanaji wa taarifa, kuendesha mijadala na kukuza ufahamu wa mambo mengi, suala la mapenzi limetajwa!

Utakutana na mtu Facebook (mfano), mmekuwa marafiki, lakini siku ya siku anaanzisha mambo ya mapenzi. Kwa sababu umeshakuwa naye karibu kwa muda mrefu, umekuwa wazi kwake ni rahisi kuanguka!
Hisia za mapenzi wakati mwingine hudanganya. Ngoja niwaambie ukweli, unapokuwa unawasiliana sana na mtu wa jinsi tofauti na yako, hisia za mapenzi huwa kali sana, kiasi kwamba ukiambiwa tu unapendwa, ni rahisi kuingia mkenge!

Kwenye mitandao ya kijamii kwa mfano Facebook, BBM, Twitter na mingineyo maarufu kuna utamaduni wa kuweka picha. Wakati mwingine picha hudanganya...kwa haraka haraka mtu eti anasema amekupenda. Hakuna lolote zaidi ya kuwaza ngono tu!
Huo ndiyo ukweli. Tatizo ni kwamba, huwezi kujua kama kuna hatari hiyo mbele yako. Unao marafiki wengi, mnataniana kila wakati, siku akilianzisha, inakuwa ngumu kuchomoka. Hata hivyo, kuna mambo madogo sana ukiyafanya yatasaidia kukutoa kwenye mtego.
Utakuta mtu ana mpenzi wake, mke au mume. Kifupi yupo kwenye uhusiano, lakini kwenye mtandao anaandika yupo ‘single’. Kwa nini hutaki kujulikana kuwa upo kwenye uhusiano?
Hujiamini? Humpendi mpenzi wako au tatizo ni nini hasa? Rafiki zako wanapoona huna mtu kwenye maelezo yako, wanatumia nafasi hiyo kukutega. Kwa nini ujiweke kwenye mitego? Kama upo kwenye uhusiano, kuwa mkweli, andika.
Ikiwezekana sehemu ya kuweka picha yako, weka ya mpenzi wako au mliyopiga pamoja, hii itasaidia marafiki kukuheshimu na wale wenye tabia za kipuuzi kujitoa mapema.
Wanaotumia mitandao ya kijamii ni mashahidi wa hiki ninachokizungumzia hapa.

MAVAZI
Kipengele hiki kinawagusa zaidi wanawake. Mavazi yanazungumza! Ulivyovaa ndivyo unavyojitafsirisha kwa wanaokutazama. Inawezekana ukawa ni mwaminifu kwa mwenzako na unajitahidi sana kuhakikisha unakuwa katika hali hiyo, lakini mavazi yako yanaweza kukutibulia.

Kwa nini uvae nguo zinazoonesha maungo yako ya ndani? Mchumba au mke wa mtu, kwa nini uvae vinguo vya ovyo? Unamwonesha nani sasa huko barabarani? Ndugu zangu, sijawahi kuona mwanamke aliyevaa kiheshima akapata usumbufu kwa wanaume njiani.
Hata kama unajijua huwezi kutegeka, lakini nataka kukuhakikishia kwamba, kusumbuliwa sana ni njia ya kuelekea kwenye usaliti. Ipo mifano hai; Kuna dada mmoja alikuwa anavaa vinguo vya kubana, kila akipita anasumbuliwa na mwanaume fulani hivi mtaani kwao.

Ameshamtumia watu mara nyingi, lakini anakataa. Siku moja ikatokea amehitilafiana na mpenzi wake, kwa hasira akaamini kuwa ameshaachana naye na hamtaki tena. Alipopita ile sehemu, yule jamaa akamuita.
Akilini mwake, akaona hakuna sababu ya kumtesa yule jamaa wakati amegombana na mpenzi wake. Kwa lengo la kujiliwaza akaenda, jamaa alilala naye siku hiyo hiyo! Alijuta baada ya kumaliza tendo!
Ya nini yote hayo? Vaa mavazi ya heshima. Jisogeze kwenye uaminifu. Ni nani atakayekusumbua ikiwa mavazi yako yanaonesha heshima uliyonayo?
Usikose wiki ijayo katika sehemu ya mwisho, kuna mambo mengi ya muhimu unayotakiwa kujua.

Friday, May 20, 2016

NEW MUSIC VIDEO: Shilole ft Barnaba - Say my name ( Watch Official Video )

Shilole a.k.a Shishi Baby kwa kushirikiana na Barnaba wanatualika kutazama video yao mpya ‘Say My Name’ na ukishaitazama uiache comment yako....