Sunday, February 12, 2017

Breaking News: Yusuph Manji Abebwa Kwenye Gari La Wagonjwa


Huyu ni mfanyabiashara maarufu wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Club ya soka ya Yanga Yusuph Manji ni miongoni mwa Watu 65 waliotajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenye orodha ya sakata la dawa za kulevya.
Manji ambaye alikwenda Polisi toka Alhamisi iliyopita, leo jioni ameonekana na Waandishi wa habari nje ya kituo cha Polisi kati Dar es salaam akichukuliwa na gari la Wagonjwa lenye namba za usajili za DFP na kuondoka nae.
Kwenye msafara huo ulioondoka gari lake aina ya Range Rover lilikuwepo pia lakini yeye alichukuliwa na gari la Wagonjwa lenye namba za usajili za DFP
Kaa nami kwa ripoti zaidi...............

No comments:

Post a Comment