Saturday, October 8, 2016

KOMBE LA DUNIA 2018 - ULAYA: FRANCE 4, HOLLAND 4, BELGIUM 4, RONALDO 4, PORTUGAL 6!

Mechi za Makundi ya Nchi za Ulaya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za huko Russia Mwaka 2018 zimeendelea Ijumaa Usiku na Mabingwa wa Ulaya Portugal kurejea kwenye reli baada ya kupoteza Mechi yao ya kwanza kwa kuitwanga Andorra 6-0 huko Mchezaji Bora Ulaya Cristiano Ronaldo akibandika Bao 4.

ULAYA – KOMBE LA DUNIA 2018
Ijumaa Oktoba 7
KUNDI A
France 4 Bulgaria 1          
Luxembourg 0 Sweden 1            
Netherlands 4 Belarus 1             
KUNDI B
Hungary 2 Switzerland 3            
Latvia 0 Faroe Islands 2             
Portugal 6 Andorra 0                  
KUNDI H
Belgium 4 Bosnia-Herzegovina 0           
Estonia 4 Gibraltar 0                  
Greece 2 Cyprus 0           

Hadi Mapumziko Portugal, waliokuwa kwao, walikuwa mbele 3-0 kwa Bao 2 za Ronaldo, aliekuwa akicheza Mechi yake ya kwanza ya kampeni hii baada kuumia, na jingine kufungwa na Joao Cancelo.
Kipindi cha Pili Ronaldo aliongeza 2 na moja kufungwa na Andre Silva.
Katika Mechi nyingine za Leo France waliifunga Hungary 4-1 kwa Bao za Kevin Gameiro, Bao 2, Antoine Griezmann na Dimitri Payet wakati Hungary walifunga kwa Penati ya Mikail Aleksandrov.

JE WAJUA?
-Ulaya itakuwa na Nafasi 13 kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia
-Washindi wa Makundi 9 watatinga moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia
-Washindi wa Pili 8 wa Makundi watacheza Mechi za Mchujo kupata Washindi Wanne kwenda Fainali za Kombe la Dunia

Nao Netherlands waliichapa Belarus 4-1 na Wafungaji wao walikuwa Quincy Promes, Bao 2, Davy Klaassen na Vincent Janssen wakati Belarus wakipata kupitia Aleksey Rios.
Belgium waliinyuka Bosnia-Herzegovina 4-0 kwa Bao za Emir Saphic, aliejifunga mwenyewe, Eden Hazard, Toby Alderweireld na Romelu Lukaku.
Jumamosi zipo Mechi 9 za Makundi C, E na F ambapo Mabingwa wa Dunia Germany watacheza na Czech Republic katika Kundi C na England kuwa kwao Wembley kucheza na Malta kwenye Kundi F.
ULAYA – KOMBE LA DUNIA 2018
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa
Jumamosi Oktoba 8
KUNDI C
1900 Azerbaijan v Norway          
Germany v Czech Republic          
Northern Ireland v San Marino              
KUNDI E
1900 Armenia v Romania            
1900 Montenegro v Kazakhstan            
Poland v Denmark            
KUNDI F
1900 England v Malta                
Scotland v Lithuania         
Slovenia v Slovakia          
Jumapili Oktoba 9
KUNDI D
1900 Wales v Georgia                
Moldova v Republic of Ireland               
Serbia v Austria               
KUNDI G
1900 Israel v Liechtenstein         
Albania v Spain                
Macedonia v Italy            
KUNDI I
1900 Finland v Croatia               
1900 Ukraine v Kosovo              
Iceland v Turkey              
Jumatatu Oktoba 10
KUNDI A
Belarus v Luxembourg                
Netherlands v France                 
Sweden v Bulgaria            
KUNDI B
Andorra v Switzerland              
Faroe Islands v Portugal             
Latvia v Hungary              
KUNDI H
Bosnia-Herzegovina v Cyprus                
Estonia v Greece              
Gibraltar v Belgium           
Jumanne Oktoba 11
KUNDI C
Czech Republic v Azerbaijan                 
Germany v Northern Ireland                 
Norway v San Marino                 
KUNDI E
1900 Kazakhstan v Romania                 
Denmark v Montenegro              
Poland v Armenia             
KUNDI F
Lithuania v Malta             
Slovakia v Scotland          
Slovenia v England.

No comments:

Post a Comment