Sunday, October 9, 2016

John McCain na Condoleezza Rice wajiondoa kumuunga mkono Trump kwenye uchaguzi huko Marekani

trump
Viongozi zaidi wa juu wa chama cha Republican, wamejiondoa kumuunga mkono mgombea urais wa Marekani wa chama hicho, Donald Trump baada ya maneno ya dharau aliyoyasema dhidi ya wanawake miaka 10 iliyopita kuvuja.
Zaidi ya viongozi 10 wa chama hicho wamesema hawatampigia kura Trump tangu kauli hiyo isambae kuanzia Ijumaaa. Trump anasema katu hatojiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho na kwamba hatowaangusha wafuasi wake.
Amekuwa kwenye kiti moto tangu video ya mwaka 2005 kuvuja akisikika akiongea kuhusu kuwabusu wanawake na kuwashika sehemu zao za siri.
Viongozi wa Republican waliojiondoa kumuunga mkono ni pamoja na mgombea wa zamani wa kiti hicho John McCain na waziri wa zamani mambo ya nje, Condoleezza Rice.
McCain amesema kauli ya Trump inafanya ishindikane kumuunga mkono kwenye harakati zake. Naye Bi, Rice amesema: “Enough! Donald Trump should not be President. He should withdraw.”
Seneta wa New Hampshire, Kelly Ayotte amesema kwenye maelezo yake: I cannot and will not support a candidate for president who brags about degrading and assaulting women.”
Mke wa Trump, Melania naye alitoa maelezo Jumamosi akisema: The words my husband used are unacceptable and offensive to me.” Hata hivyo alimtetea akidai kuwa mumewe ana moyo na fikira za kiongozi.

No comments:

Post a Comment