Tuesday, October 11, 2016

Ujerumani wamefanya jambo kwaajili ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere

Leo October 11 2016 BBC wameripoti taarifa ya Chancellor  wa Ujerumani Angela Merkel kuzindua jumba jipya la makao makuu ya Umoja wa Afrika ambalo limepewa jina la baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuelekea siku ya kumbukumbu tarehe 14.
Jumba hilo ambalo jina lake kamili ni Jumba la Amani na Usalama la Julius Nyererelimejengwa kwa ufadhili kutoka Ujerumani, litakuwa makao ya idara ya Amani na Usalama ya AU na litatumiwa pia na maafisa wa kutoa tahadhari ya mapema kuhusu mizozo barani pamoja na kuratibu juhudi za kulinda amani za AU.Ujenzi wa jumba hilo, ambalo ukubwa wake wa sakafu ni mita 13,500 mraba na linaweza kutumiwa na wafanyakazi 360, uligharimu euro milioni 27. Jumba hilo ofisi za kufanyia kazi, vyumba vya mikutano vya kutumiwa na Baraza la Amani na Usalama, chumba cha kuratibia shughuli, maktaba na vyumba vya shughuli za pembeni.Mwalimu Nyerere, ambaye alikuwa rais wa Tanzania hadi 1985, alikuwa mmoja wa viongozi waanzilishi wa Muungano wa Nchi za Afrika (OAU) ambao sasa ni Umoja wa Afrika (AU). Alishiriki sana katika jitihada za kuendeleza bara la Afrika na kusaidia mataifa ambayo hayakuwa yamepata uhuru kujipatia uhuru wake.

No comments:

Post a Comment