Saturday, October 8, 2016

Chris Brown aharibu simu ya shabiki wake mombasa, kisa ni Selfie!

Msanii wa RnB kutokea Marekani ambaye wengi tunamfahamu kutokana na umaarufu mkubwa alio nao, Chris Brown amemfanyia shabiki wake kitendo ambacho kimeleta tafsiri mbaya nchini Kenya.
Ikiwa ni kuelekea show ambayo ataifanya nchini humo, waandishi wa habari wamezungumza na shabiki ambaye amefahamika kwa jina la Brenda ambaye anasema kuwa alikuwa akielekea kumpokea mgeni wake uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Moi akiwa na dada yake ndipo alipomuona msanii huyo na kumfuata kumuomba apige naye Selfie.

Brenda anasema alipojaribu kumwomba Chris apige naye picha, Chris hakujibu lolote ndipo alipomtangulia kwa mbele akijaribu kufanya jitihada za kulazimisha haja yake kutokana na mapenzi aliyo nayo kwa msanii huyo.

Brenda anasema jitihada zake ziligonga mwamba baada ya Chris kunyakua simu yake na kuitupa chini huku akitanabaisha kuwa simu yake ni Iphone 6 ina gharama ya Shilingi 81,999 kwa pesa za Kenya.

Brenda anasema alikuwa anampenda sana Chris Brown na alipania sana kuwepo kwenye hiyo show lakini kutokana na kitendo hicho hatoweza kuhudhuria.

Tukio hili linatokea baada ya lile la msanii Koffi Olomide kumpiga kibao mmoja kati ya wafanyakazi wa bendi yake hukohuko nchini Kenya uwanja wa ndege wa JKIA.

No comments:

Post a Comment