Tuesday, October 11, 2016

Misaada zaidi yatolewa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa leo (Jumanne) oktoba 11, 2016, amepokea misaada mbalimbali kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi kutoka Ubalozi wa Japan, Shirika la Jica na kampuni mbalimbali ya hapa nchini.Misaada iliyotolewa ni pamoja na mahema 220, mablanketi 1100, magodoro 1100, ndoo 250 pamoja na fedha taslimu kiasi cha Sh376 milioni.Taasisi nyingine zilizochangia ni Shirika la Utangazaji (TBC), kampuni ya Acacia, Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, Sura Technologies na Umoja wa Mafundi Gereji Kinondoni.Waziri Mkuu amewashukuru wote waliochangia na kusema tayari Serikali imemruhusu mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya mkoa wa Kagera kuanza kutumia fedha zilipo kwenye akaunti ya maafa kagera kwa kadri ya mahitaji.

No comments:

Post a Comment