Showing posts with label Habari za jamii. Show all posts
Showing posts with label Habari za jamii. Show all posts

Wednesday, February 8, 2017

VIDEO: Kumbe Yule Mama Mjane Aliyelia Mbele Ya Rais Magufuli Ni Mwongo, Jipya Laibuka ( Hot News )

YOU recall the woman who appeared before the President Magufuli crying for help in matters of inheritance, where he said he wants kudhurumiwa to lawyers and relatives?

Brother happened to the legitimate wife of the deceased and these are new they say, 

See video....

Monday, January 30, 2017

Kutana na Mfungwa aliyefaulu Shule Gerezani na sasa atakwenda chuo kikuu London

Inatokea kwenye gereza la Naivasha Kenya ambapo Mfungwa Michael Kahiga ni miongoni mwa Wafungwa wachache watakaojiunga na chuo kikuu kutokana na jitihada zake za kujisomea kwa bidii chini ya Mwalimu wake pia ambaye pia ni Mfungwa wa kifungo cha maisha.
Kwenye gereza hilo la Naivasha kuna Liblary ambayo ina vitabu mbalimbali ambapo Michael anasema pamoja na yeye kufaulu kwenda chuo kikuu, kwenye kusoma kwake akiwa gerezani bado hakuwa na Waalimu ambao wamekidhi vigezo.
Michael anatumikia kifungo cha miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya wizi ambapo baada ya kumaliza kifungo chake, atajiunga na chuo kikuu cha London Uingereza ambacho kimempa nafasi ya kusoma bure kwenye chuo hicho baada ya kufaulu vizuri kwenye mtihani wa kitaifa gerezani.
Kwa mujibu wa K 24 Kenya, kwenye mtihani aliofaulu Michael ni Wanafunzi 141 walipata A ambapo Michael mwenyewe alipata C+, unaweza kumtazama kwenye hii video hapa chini.

Saturday, January 28, 2017

Majambazi Wawili Wauawa Huku Wauza Shisha Wakiwekwa Chini Ya Ulinzi

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewaua watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi na kukamata silaha pamoja na watuhumiwa kadhaa wa matukio ya kihalifu wakiwemo 7 wanaotuhumiwa kutengeneza kadi 7 za bandia za chanjo ya homa ya manjano

Akizungumza na vyombo vya habari, jana Jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro alisema, mnamo tarehe 23 mwezi wa kwanza mwaka 2017 majambazi hao walitekeleza tukio la mauaji na kupora kiasi cha shilingi milioni 1 na laki 3 huko Boko Basihaya na polisi iliwasaka na kuwakamata na wakakiri kutenda mauaji hayo na kwamba walipojaribu kutoroka ndipo walipouawa.

Akielezea kukamatwa kwa watu 7 wanaodaiwa kutengeneza kadi bandia za homa ya manjano ambazo mtu hupaswa kuchomwa chanjo hiyo kabla ya kusafiri nje ya nchi, Kamisha Sirro alisema, watu hao wamekuwa wakitoa kadi hizo na kudai fedha nyingi kinyume cha sheria.
Kamanda Sirro akionesha mkasi unaotumiwa na wahalifu kuvunja vitu mbalimbali

Jeshi hilo pia limewakamata watuhumiwa 92 wa makosa mbalimbali, ikiwemo wizi wa magari na pikipiki, watengenezaji wa gongo, shisha na uuzaji wa bangi.

Pia limekusanya zaidi ya Shilingi milioni 918, kwa ukamataji wa makosa ya usalama barabarani katika kipindi cha siku 10.
Kamanda Sirro akionesha magari yaliyokuwa yameibiwa katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam

Friday, January 27, 2017

Geita: Watu 14 wafukiwa na kifusi mgodini


Watu kumi na nne wamefukiwa na udongo Alhamisi hii baada ya mgodi mmoja kuporomoka katika mkoa wa Geita, walipokuwa wakiendelea na uchimbaji wa madini.
Watu hao ni raia 13 Watanzania na raia mmoja wa China. Tukio hilo limetokea saa 9 usiku leo (jana) wakati wachimbaji hao wakiendelea na shughuli ya uchimbaji katika mgodi wa RZ unaomilikiwa na wachina.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga ametembelea eneo la tukio na kuona shughuli za uokozi zikiendelea na kuagiza nguvu ziongezwe.
Inaelezwa kuwa udongo umeporomoka kutokana na mgodi kuchimbwa zamani na Wajerumani hivyo kusababisha baadhi ya maeneo hayo kuwa na nyufa na vyuma kushindwa kushikilia udongo wa juu hali ambayo imesababisha kuzidiwa na hatimaye kuporomoka.
Kamisha msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria Mhandisi Yahaya Samamba amesema jitihada zilizofanyika ni kuwasiliana na migodi iliyopo karibu na eneo hilo pia wameomba msaada kutoka Kahama na kwenye mgodi wa GGM kupatiwa vifaa vya uokoaji ili zoezi hilo liweze kufanikiwa.
“Jitihada ambazo tumezifanya hadi sasa tumeomba msaada Kahama na kwenye mgodi wa Geita,kupatiwa vifaa ambavyo vitasaidia kwa wepesi zoezi hili la uokoaji ingawa tumeshapata vifaa vingine kutoka kwenye mgodi wa Busolwa”,alisema Samamba.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Geita Elisa Mugisha amesema eneo la chini ambalo limefukiwa na udongo ndiyo ambalo sasa wanaendelea kulitanua ili sehemu hiyo iwe kubwa watu waweze kupita.
“Eneo lote lile la chini limefukiwa na udongo lakini kule chini kunaonekana kuna sehemu za kwenda pembeni ingawa limefukiwa lakini chini kuna uimara kuna uwezekano kule chini wale watu wapo hai na wamepelekewa mipira ya hewa na kazi inayofanyika ni kutanua eneo ambalo litasaidia kuwatoa watu hao”,amesema.
Mwanasheria na msemaji wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya RZ Frances Kiganga ameelezea kuwa chanzo kikubwa ni mashimo ya zamani kwani udongo unapotikisika umekuwa ukisababisha baadhi ya nyufa kuendelea kupata shida.

Friday, October 14, 2016

Isikupite hii ya diwani wa Chadema kunaswa na dawa za kulevya pamoja na bunduki


Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa linamshikilia Diwani wa kata ya Izira, Paschael Silimba (Chadema) baada ya kumkamata akiwa na dawa za kulevya aina ya bangi na bunduki moja aina ya gobole.
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, George Kyando amesema kuwa jeshi hilo lilimkamata Kyando katika eneo la soko kuu ambalo hufanyia biashara yake ya kuuza mifuko ya salfeti, baada ya kupata taarifa na kuamua kumfuatilia.
Alisema kuwa baada ya kumpekua katika vifurushi vya bidhaa hiyo anayoiuza kwa kushirikiana na mkewe, walibaini uwepo wa bangi kiasi cha robo kilo.
“Baada ya kufanya upekuzi kwenye duka la diwani huyo, tumefanikiwa kukamata bangi kiasi cha robo kilo. Ni bangi kavu ambayo imeshaandaliwa tayari kwa ajili ya kufanya packing na kuuzwa,” alisema Kamanda Kyando.
Akizungumzia silaha aina ya gobole waliyoikuta nyumbani kwa diwani huyo anayodaiwa kuimiliki kinyume cha sheria, alisema ingawa ni silaha ya kizamani ina nguvu ya kuua tembo.
“Silaha hii ina nguvu sana, ina uwezo wa kuua tembo na ni hatari sana akipigwa binadamu kwa silaha hii. Kwahiyo msiione hapa mkaidharau, ina nguvu sana,” aliongeza.
Kamanda Kyando aliwataka viongozi wote waliopewa dhamana na wananchi kutotumia nyadhifa zao kufanya uhalifu. Alitoa wito wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kufichua uhalifu bila kujali waliofanya uhalifu huo.

Wednesday, October 12, 2016

Mwalimu aliyemtukana mwanafunzi wa kidato cha sita Iringa, Mahakama imetoa maamuzi!


Ikiwa matukio ya unyanyasaji mashuleni yakiendelea kutokea, Mahakama ya Mwanzo Iringa  Mjini imemuachia huru mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kiwele baada ya kukosa ushahidi wa kumtia hatiani katika kesi ya  kumtukana mwanafunzi.
Mwalimu huyo, Elizabeth Maliga (32) ameshtakiwa kwa madai ya kumtukana mwanafunzi huyo wa kidato cha sita, Rehema Mwakatobe na mama yake.
Amedaiwa kufanya kosa hilo wakati akimsainia Rehema barua ya kumuita mama yake kwenda shuleni hapo kusikiliza kosa la kuchelewa shuleni.
Hukumu hiyo imetolewa wakati Taifa likiwa kwenye mjadala mkubwa baada ya picha za video zilizosambaa mitandaoni kuonyesha kundi la walimu wa Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya likimshambulia mwanafunzi Sestian Chikungu.
Tayari Serikali imeshatangaza kuwafukuza chuo walimu hao na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi.
Akisoma hukumu ya kesi hiyo iliyochukua takriban dakika 45, Hakimu wa Mahakama hiyo,  Abdallah Kutvai alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuishawishi mahakama kumtia hatiani mshtakiwa huyo.
“Jukumu la kuthibitisha kosa ni la upande wa mashtaka. Hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha tano cha Sheria ya Ushahidi ya Mahakama ya Mwanzo iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
“Mashahidi wa upande wa mashtaka wametofuatiana tarehe za kutendwa kosa hilo. Shahidi namba moja ambaye ni mlalamikaji anasema kosa limetendeka Septemba 13, mwaka huu kwenye kikao cha kujadili mwenendo wa utekelezaji wa adhabu zilizotolewa na walimu kwa wanafunzi shuleni hapo,”alisema Hakimu Kutvai.
Amefafanua kuwa shahidi namba mbili alishindwa kubainisha siku ya tukio na kutaja tarehe tatu tofauti, ambazo ni Septemba 13, 14 na 15, siku ambayo mwanafunzi huyo alipewa barua ya kurudishwa nyumbani kwao Dar es Salaam kumfuata mzazi.

Ni kweli kuna uhaba wa dawa vituo vya afya, Serikali imekiri

Makamu  wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amekiri kuwapo  uhaba wa dawa   na vifaa tiba katika hospitali za Serikali nchini.
Amesema uhaba huo wa dawa ni changamoto ya muda mfupi na Serikali inatafuta ufumbuzi wa haraka  kuwahudumia wananchi.
Alikuwa akizungumza  Dar es Salaam jana wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa wodi ya kina mama na watoto katika hospitali zote za rufaa  za Mkoa wa Dar es Salaam.
Samia alisema anatambua changamoto zinazoikabili Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kwamba ni ukosefu wa dawa.
“Natambua katika hospitali zetu za rufaa tuna changamoto ya vifaa tiba na dawa, lakini Serikali tunaifanyia kazi  kila mwananchi aweze kupata huduma hizo kama ilivyopangwa,”alisema.
Alisema   idadi watu wanaoongezeka katika Mkoa wa Dar es Salaam husababisha msongamano wa wajawazito na watoto katika hospitali za Serikali na kuwafanya kina mama walale chini au walale mbali na watoto wao.
“Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, takriban wanawake 432 kati ya vizazi hai 100,000, hufa kila mwaka kutokana na uzazi na asilimia 80 ya vifo hivyo husababishwa na ukosefu wa vifaa tiba, umbali wa vituo vya afya, upasuaji wa huduma za dharura ya upasuaji kwa wajawazito na kuongezewa damu.
“Kwa Mkoa wa Dar es Salaam peke yake, kuna zaidi ya hospitali 42 zinazotoa huduma za dharura za uzazi kwa kasi ya ukuaji wa jiji na bado Serikali inahitaji zaidi ya hospitali 30 ndani ya miaka 10 ijayo,” alisema.
Kwa mujibu wa Samia, mradi wa ujenzi huo utagharimu Sh bilioni 4.5 kwa hospitali tatu na kila hospitali yenye ghorofa tatu  na uwezo wa kuwekwa vitanda 150, itagharimu Sh bilioni 1.2.
Alisema Serikali imejipanga kuhakikisha hospitali zote za rufaa zinaendelea kuimarishwa ili kutoa huduma bora za afya ikiwamo afya ya mama na mtoto.

Pesa za kutumika kwenye mwenge zitatumiwa kwa matumizi mengine, uwepo wa viongozi pia vipi?

Kuna taarifa ktoka Ikulu Dar es Salaam ambapo katibu mkuu kiongozi balozi John Kijazi ameeleza kuwa Rais Magufuli ameagiza viongozi wote wa serikali walioalikwa kuhudhuria sherehe za kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa 14 Oktoba Bariadi Simiyu kutohudhuria sherehe hizo na wale ambao walishalipwa fedha ya posho na safari wazirejeshe.President ametoa maagizo hayo ikiwa ni utekelezaji wa azma ya serikali ya awamu ya tano ya kubana matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza rasilimali nyingi katika shughuli za maendeleo ya nchi.Viongozi waliotajwa kutakiwa kufuta safari zao za kwenda Bariadi ni pamoja na wakuu wote wa mikoa, wakuu wote wa wilaya, wakurugenzi wote wa mamlaka za serikali za mitaa, mameya na wenyeviti wote wa Halmashauri za majiji, manispaa, miji na wilaya pamoja na watumishi ambao huambatana nao wakiwemo madereva na wasaidizi wao ambao kwa idadi hufikia takribani 1,500.Kwa kuwa sherehe za kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru huambatana na maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki miaka 17 iliyopita, agizo hilo limewataka viongozi wote wa mikoa na wilaya kubaki katika maeneo yao ya kazi na kujiwekea utaratibu wa jinsi ya kuienzi siku hiyo.Aidha, Rais Magufuli ameagiza wilaya zote ambazo zimefanya vizuri katika shughuli za maendeleo wakati Mwenge ulipokuwa katika maeneo yao, zitambuliwe kwa kutangazwa rasmi katika siku ya kilele cha mbio za Mwenge na kwamba zawadi zilizoandaliwa zitapelekwa kwa wahusika kwa utaratibu utakaoelekezwa na mamlaka inayohusika kutoa zawadi hizo.Hata hivyo Dkt. Magufuli ameelekeza kuwa kutokana na umuhimu wa mwenge wa Uhuru kwa Taifa, Viongozi wote wa serikali ya mkoa wa simiyu na wilaya zake pamoja na wananchi wote wa mkoa huo wajitokeze kwa wingi na kushiriki katika sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru siku hiyo ya tarehe 14 Oktoba, 2016.Mgeni Rasmi katika sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru atakuwa Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein

Tuesday, October 11, 2016

Misaada zaidi yatolewa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa leo (Jumanne) oktoba 11, 2016, amepokea misaada mbalimbali kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi kutoka Ubalozi wa Japan, Shirika la Jica na kampuni mbalimbali ya hapa nchini.Misaada iliyotolewa ni pamoja na mahema 220, mablanketi 1100, magodoro 1100, ndoo 250 pamoja na fedha taslimu kiasi cha Sh376 milioni.Taasisi nyingine zilizochangia ni Shirika la Utangazaji (TBC), kampuni ya Acacia, Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, Sura Technologies na Umoja wa Mafundi Gereji Kinondoni.Waziri Mkuu amewashukuru wote waliochangia na kusema tayari Serikali imemruhusu mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya mkoa wa Kagera kuanza kutumia fedha zilipo kwenye akaunti ya maafa kagera kwa kadri ya mahitaji.

Wafungwa 472 wasubiri hatma yao kutoka kwa Rais Magufuli, Adhabu ya kunyongwa ina takwimu zake pia

Watu 472 waliohukumiwa adhabu ya kifo kutokana na makosa mbalimbali, wanasubiri saini ya Rais Dk. John Magufuli ili kujua hatima ya utekelezaji wa adhabu zao ama laa.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa kati ya watu hao, wanaume ni 452 na wanawake ni 20. Taarifa hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu adhabu ya kifo.
Bisimba alisema, watu hao walihukumiwa adhabu ya kifo kutokana na kutiwa hatiani na makakama kwa makosa ya uhaini na mauji.
Licha ya adhabu hiyo alisema hatua ya utekelezaji wake inakwenda kinyume na haki za binadamu kama inavyotafsiriwa katika matamko na mikataba mbalimbali ya kimataifa.
Kutokana na hali hiyo, Dk. Kijo-Bisimba, alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana, jumla ya watu 472 walikuwa wamehukumiwa adhabu hiyo.
Alisema wakati watu hao wakisubiri adhabu hiyo, wengine 244 waliopo katika magereza mbalimbali bado wanasubiria maamuzi ya rufaa zao.
“Licha ya adhabu hii kutotekelezwa hapa nchini kwa takriban miaka 22 na miaka 24 ya kwanza ya uhuru, taarifa zinaonesha kuwa hadi sasa ni watu 72 tu ambao wameshanyongwa kutokana na adhabu hiyo,”alisema.
Dk. Kijo-Bisimba alitoa taarifa hiyo katika kipindi cha kuelekea maadhimisho ya siku ya kupinga adhabu ya vifo duniani, ambayo itafanyika katika nchi 70 na kaulimbiu ikiwa ni “Kuua ni Nyenzo ya Kigaidi, Acha Mnyororo wa Kigaidi,”.
“Leo ni miaka 14 tangu wanaharakati walivyoamua kuwepo kwa siku hii tusipokuwa na uhai hatuwezi kufanya kitu chochote hivyo adhabu hii haina maana kwani inaingilia haki ya uhai wa binadamu na kuona si kitu cha thamani,” alisema Bisimba.
Mkurugenzi huyo alisema, hadi sasa nchi 140 duniani zimeshafuta adhabu hiyo, ambapo kwa upande wa Afrika nchi 17 zimeshakubali kufuta adhabu hiyo.
Hata hivyo alisema ni wakati mwafaka kwa Serikali kuondoa adhabu hiyo, ili Tanzania iwe nchi ya 18 katika bara la Afrika kufuta adhabu hiyo, ambayo haina faida yoyote.
Mkurugenzi huyo wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, alisema kuwa adhabu hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa ikiwamo kuwapa marais ugumu kuweka saini kwa mtu kuuawa.
“Ni miaka 22 sasa nchi yetu haijawahi kutekeleza adhabu hiyo kwani Rais ndiye anayeruhusiwa kwa mujibu wa sheria lakini hata wao wanaogopa kufanya hivyo ili mtu mwingine afe badala yake wangetoa adhabu mbadala kwani wengine wanaofanya makosa hayo ni vichaa,”alisema.
Alisema adhabu hiyo ni ya kibaguzi na huwatia hatiani watu maskini wasiokuwa na uwezo wa kujitetea mahakamani au kuweka mawakili.
Dk. Bisimba, ameiomba Serikali isitunge tena sheria ya kifo na ikiwezekana ya sasa ikiwemo iliyoongezwa ya makosa ya ugaidi iondolewe na kutafutwa adhabu mbadala kwa mtu atakayetiwa hatiani.
“Adhabu ya kifo imeainishwa kwenye Sheria ya Kanuni ya Adhabu, sura ya 16 ‘Penal Code’ ambayo ililetwa na utawala wa kikoloni mwaka 1945. Hata baada ya Uhuru 1961 hukumu ya kifo imeendelea kuwa sehemu ya sheria licha ya marekebisho mbalimbali ya sheria hiyo ikiwemo marekebisho ya mwaka 2002. “Adhabu ya kifo hutolewa kwenye makosa ya mauaji chini ya sheria hiyo kifungu 197 na kwenye hati ya kosa la uhaini chini ya kifungu cha 39 (3) (C).
“Pamoja na hayo mwaka huu Serikali imeongeza adhabu ya kifo kama mtu akikutwa na kosa la ugaidi chini ya sheria ya kudhibiti ugaidi ya mwaka 2002 kwenye mabadiliko madogo ya sheria, hii imeengeza makosa ambayo mtu anaweza kuhukumiwa kifo kufikia makosa matatu,”alisema Dk. Bisimba
Alisema kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu na mikataba mbalimbali ya kikanda na kimataifa ya haki za binadamu, zipo sababu za msingi za kupinga adhabu ya kifo.
“Tunapenda kuweka wazi kuwa hatufurahii watu kuua watu wengine na ndiyo maana hatungependa hata muuaji auawe kwa vile ni sawa na kumkubalia kuua. Adhabu ya kifo ni ya kinyama na isiyo na staha, inayotweza utu wa ubinadamu na hufanya Serikali ionekane pia kama mhalifu kwa kuua.
“Adhabu hii ikitolewa kwa mtu asiye na hatia kimakosa huwezi kuirekebisha kwani mfumo wa utoaji haki huwa pia na mianya ya makosa na hivyo maisha ya mtu yanweza kupotea bure na hakuna ushahidi kama adhabu hii inazuia watu wengine kutotenda makosa kama hayo,” alisema
Mbali na maadhimisho hayo kituo hicho kilizindua kitabu kinachoelezea adhabu ya kifo na ukiukwaji wa Haki za Binadamu cha mwaka 2015.

Polisi wajeruhi watuhumiwa wa ujambazi Dar

Watuhumiwa wawili kati ya watano wa ujambazi wamejeruhiwa katika majibizano ya risasi na jeshi la polisi na kutiwa mbaroni katika eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam,baada ya kueleza lilikuwa jaribio la kupora fedha katika kiwanda kimoja. Katika tukio hilo watuhumiwa watatu wamefanikiwa kutoroka.Taarifa hiyo imetolewa na kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, kamanda Simon Sirro.“Polisi wa jiji la Dar es Salaam waliwahi eneo na wakafanya mtego na kweli bahati nzuri walifanikiwa,kabla wale majambazi hawajafanya tukio walifanikiwa kuwarushia risasi,kwa maana ya kutaka wasimame, lakini na wao hawakukubali kusimama,” alieleza Sirro.“Kwahiyo polisi walipiga risasi juu na walipoona mwisho wa siku wakapotea, wakaweza kuwapiga risasi majambazi wawili na walipokwenda kuwapekua ndio walikuta hii silaha ya aina ya MARK IV.”

Kuhusu uwepo wa dawa nchini Wizara ya Afya yatoa ufafanuzi

Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa katika baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii vikizungumzia hali ya dawa nchini hasa kufuatia taarifa zilizotolewa na taasisi ya kiraia na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa.
Taarifa hizo zilidai kwamba katika kipindi hiki kuna upungufu mkubwa wa dawa katika bohari kuu ya dawa , Hivyo, kusababisha kukosekana kwa dawa katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
Taarifa hizi si sahihi na zinalenga kupotosha umma na kuwatia wananchi wasiwasi. Napenda kuwathibitishia wananchi kuwa Afya ni suala la kipaumbele kwa Serikali ya Awamu ya Tano. Hivyo, ningependa kutoa ufafanuzi kwa wananchi katika masuala yafuatayo; –
Hali ya Upatikanaji wa dawaHali ya upatikanaji wa dawa kwa sasa iko vizuri. Dawa muhimu zinazohitajika  sana nchini zinapatikana kwenye maghala ya Bohari ya Dawa (MSD). Mfano kwa upande wa dawa za antibiotics tuna Amoxycillin, Ciprofloxacin, Cotrimoxazole na Doxycycline. Kwa upande wa dawa za maumivu – tunazo za kutosha kama vile paracetamol, asprin na diclofenac.
Pia tuna dawa za kutosha za malaria, Kifua Kikuu, ukoma na dawa za kufubaza makali ya UKIMWI (ARVs). Kwa upande wa chanjo za watoto na wajawazito, ni kweli kulikuwa na uhaba nchini kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita. 
Hata hivyo, wiki iliyopita Serikali imenunua na kupokea dozi milioni 2 za chanjo ya Kifua Kikuu (BCG), dozi milioni 1.2 za Polio na dozi milioni za Polio. Chanjo hizi zinasambazwa katika vituo vya afya nchini.
Dawa nyingine zitaendelea kupatikana katika Bohari kuu ya Dawa kwa kuwa tumeagiza dawa za kutosha kutoka kwa wazalishaji wa ndani na nje ya nchi. 
Aidha, kiasi kikubwa cha dawa zinazowasili Bohari kuu ya Dawa zikifika zinapelekwa kwenye Kanda nane za MSD pamoja na vituo viwili vya Mauzo kwa ajili ya kuwasambazia wateja walioagiza. 
Hivyo, kipimo cha upatikanaji wa dawa si kuangalia katika maghala ya Bohari ya Dawa peke yake bali pia katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Ili kuondoa mlolongo wa manunuzi ya dawa, tunapenda kuwataarifu kuwa Bohari kuu ya Dawa imepanua wigo wa upatikanaji wa dawa kwa sasa kwa kutumia mikataba ya muda mrefu (miaka miwili) na washitiri wa ziada wa ndani (Prime Vendors) ili kuhakikisha dawa zinapokosekana MSD zinapatikana kwa haraka kwa Washitiri wa ndani waliothibitishwa katika kila mkoa.
Katika muktadha huo huo, Bohari ya Dawa imefungua maduka ya ziada kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa dawa zaidi ya aina 600 kupitia mfumo wa maduka katika mahospitali kama vile Muhimbili, Mbeya na Arusha.
Bajeti ya dharura kwa ajili ya dawaNi muhimu wananchi wakajua kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya manunuzi ya dawa katika mwaka wa fedha 2016/17 zinatosha kuhudumia mahitaji ya dawa kwa mwaka mzima. Hivyo hakuna sababu ya kuwa na bajeti ya dharura.
Niwakumbushe bajeti zilizotengwa kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa tiba katika miaka michache iliyopita mpaka hivi sasa, kama ifuatavyo: -.
Mwaka 2011/2012 bajeti iliyotengwa ilikuwa shilingi Bilioni 23.7
Mwaka 2012/2013 bajeti ilikuwa shilingi Bilioni 34
Mwaka 2013/2014 ilikuwa shilingi Bilioni 34
Mwaka 2014/2015 ilikuwa shilingi Bilioni 60
Mwaka 2015/2016 ni shilingi Bilioni 30
Na mwaka huu 2016/17 ni shilingi Bilioni 251.5
Mkakati wa Wizara kwa sasa ni kuhakikisha kuwa fedha hizo zinapatikana kwa wakati kutoka Hazina kulingana na makusanyo ya nchi.
Vilevile ieleweke kwamba tayari serikali imeshatoa kiasi cha shilingi bilioni 20 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2016/17,  kwenda Bohari kuu ya Dawa kwa ajili ya ununuzi wa dawa na chanjo. Hali hii inathibitisha kuwa suala la upatikanaji wa dawa ni la kipaumbele kwa Serikali ya Awamu ya tano.
Kulipa Deni la Bohari ya Dawa (MSD)Napenda kuwafahamisha kuwa Serikali imedhamiria kulipa deni lote la Bohari ya Dawa (MSD) ambapo katika mwaka huu wa fedha 2016/17 tayari Bilioni 85 imekwishatenga kwa ajili ya kulipa deni hilo.Jambo ambalo halijawahi kutokea huko nyuma. Kulipwa kwa deni hilo kutasaidia kuhuisha mtaji wa MSD (revolving fund) na hivyo kuiwezesha MSD kuwa na dawa na vifaa tiba kwa kiwango kikubwa.
Aidha serikali imekwisha kuviagiza vituo vyote vinavyotoa huduma za Afya kupitia Halmashauri zao, kuhakikisha zinakuwa na fedha ya mzunguko kwa ajili ya kununulia dawa (revolving fund) na hivyo kupata dawa kwa kulipa fedha taslimu kutoka Bohari ya Dawa badala ya kukopa.
Fedha hizo zitapatika kutoka kwenye vyanzo vyao vingine vya mapato kama vile Bima ya Afya (NHIF, CHF) na gharama wanazochangia wananchi katika kupata huduma. Hii itawezesha kutoendelea kukuza deni kutoka Bohari ya Dawa na kuhakikisha dawa zinapatikana kwa wakati wote.
MSD Kupata MshindaniKatika mwaka 2015, Serikali ilimpa kazi mshauri mwelekezi wa kampuni ya ushauri iliyobobea kimataifa ya Deloitte ya kulitazama jambo hili kwa ajili ya kuifanyia tathmini MSD pamoja na mambo mengine ikiwemo kuangalia suala ya kutafutiwa mshindani katika manunuzi na usambazaji wa dawa.
Napenda kuwajulisha kuwa tathmini hiyo ilionyesha kuwa MSD kutafutiwa mshindani itakuwa ni kuongeza gharama kubwa kwa serikali kutokana na kurudufisha (duplication) majukumu. 
Pia ilibainika kuwa suala la dawa ni muhimu, hivyo Serikali haiwezi kuliacha kwenye mikono ya watu binafsi.Jambo ambalo lilipendekezwa ni kuifanyia maboresha makubwa MSD ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Utekelezaji wa mapendekezo hayo tayari umeshaanza.
Nchi ambazo zinaiuzia dawa na vifaa tiba MSDMSD inaagiza dawa na vifaa tiba nje ya nchi zaidi ya asilimia 80 kwa sababu viwanda vilivyoko ndani ya nchi havikidhi mahitaji ya nchi kwa ubora na kiasi. Hivyo, MSD hununua dawa na vifaa tiba kutoka nchi za India, China, Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Ujerumani, Marekani, Ufaransa na sehemu nyingine duniani.
Kwa mfano, tuna dawa zaidi ya aina  nne ambazo zinanunuliwa kutoka Kenya (Dawa ya kutibu malaria kwa akina mama wajawazito ijulikanayo kama Sulfadoxine Pyrimethamine (SP), dawa ya kutibu magonjwa ya maambukizi ya Cotrimoxazole  ya watu wazima na watoto pamoja, Amoxicilline  na Paracetamol ya maji kwa ajili ya watoto.
Ikumbukwe kuwa MSD hununua dawa hizi kupitia mchakato wa zabuni, ikiwa baadhi ya vigezo ni kuangalia usajili wa dawa nchini pamoja na ushindani wa bei. Hata hivyo, ili kukuza viwanda vya ndani, watengenezaji wa dawa wa ndani hupewa hadi 15% ya upendeleo katika mchakato wa tathmini ya zabuni dhidi ya dawa zinazotoka nje ya nchi (Domestic preference).
Kwa upande mwingine mkakati wa serikali sio kuendelea kutegemea dawa kutoka nje ya nchi, kwani kwa kufanya hivi uchumi wa nchi hautakuwa. hivyo basi serikali iko katika hatua za mwisho za utaratibu wa kuwakaribisha wawekezaji wa viwanda vya kuzalisha dawa kuwekeza nchini kwa mpango wa kuwashirikisha wadau wengine katika masuala ya dawa  (PPP).
HitimishoWizara ya afya inapenda kuwahakikishia wananchi kuwa itasimammia ipasavyo utapatinaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba nchini kwa wakati na kwa bei nafuu kwa kuwa Sera ya afya inawataka wananchi kuchangia huduma.
Aidha vituo vya kutolea huduma za Afya vinahimizwa kupeleka mahitaji na maoteo yao ya dawa kwa wakati badala ya kusubiri hadi dawa zote muhimu zimeisha kabisa katika vituo vyao. Pia wanakumbusha kulipa madeni wanayodai na bohari ya dawa sambamba na kuhakikisha fedha inayopatikana katika shughuli za utoaji huduma inatumika kwa ajili ya dawa, vifaa na vifaa tiba.
 Ili kuondoa vikwazo kwa wananchi katika kupata dawa na huduma za afya kwa ujumla wananchi wanahimizwa kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya kwani hakuna anayejua leo hama kesho ataugua na Magonjwa hayapigi hodi na wakati mwingine yanakukuta hauna  akiba ya fedha, ila ukiwa na bima wakati wowote unapata matibabu.
Mwisho, Wizara itaendelea kuhakikisha kuwa kuna dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara vya kutosha kwenye vituo vya umma vya kutolea huduma za Afya nchini

Monday, October 10, 2016

Kinachoendelea kuhusu Mwalimu Frank Msigwa na utata wa akaunti yake ya Instagram!

Baada ya kufukuzwa Chuo kwa hatua yao ya kushiriki kitendo cha kumpiga mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya kutwa ya sekondari mkoani Mbeya (Mbeya Day), Mwanafunzi Sebastian Chingulu tamko lililotolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako , Mwalimu Frank Msigwa  hatimaye ameibuka na kuomba msamaha kwa Watanzania.Frank Msigwa kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, (frank_msigwa_) ambayo hadi leo Oktoba 10.2016 akaunti hiyo imeweza kupata Followers 741 na Following  ikifikia 2065,   huku akiwa ameposti mara m ili tu ikiwemo post yake ya jana Oktoba 9 juu ya tamko lake hilo la kuomba msamaha na leo kupost tamko la kusikitishwa kwake kwa Watanzania walivyopokea msamaha wake huo. (Angalia picha).Watu mbalimbali wamekuwa wakichukulia tofauti msamaha wake huo na hata wengine wakiubeza kuwa ni akaunti ‘feki’ ya Mwalimu huyo Mwanafunzi Frank  Msigwa.Mbali na kuona suala hilo la msamaha kwa kijana huyo kupitia mitandao ya kijamii watu mbalimbali wameeleza kuwa alipaswa kwenda kwenye vituo vya radio na TV kuomba msamaha huo huku wengine wakimtaka aende kwa wazazi wa mtoto aliyepigwa ndio wataweza kumsamehe.Kwa hali hiyo hadi sasa bado Frank Msigwa anazua maswali mengi kwa wananchi kama ni kauli yakke kutoka kinywa chake ama ni mtu ameamua kufanya hivyo kwa niaba ya Msigwa?..

Huu ndio ujumbe unaodaiwa ni wa mwalimu Frank Msigwa....frank msigwa

Huyu Ndo Mwalimu Aliyerekodi Tukio la Kikatili la Kupigwa Mwanafunzi na Walimu Mbeya Day

Pichani ni mwalimu aliyechukizwa na kitendo cha walimu wanne waliomshambulia Mwanafunzi kama wamekutana na Scorpion, pia alisikika akisema "mwalimu muacheni mtamuumiza" naamini ameokoa wanafunzi wengi wanaopigwa kama nyoka mashuleni bila sisi

Katika kukomesha suala la dawa za kulevya, mbinu mpya zimegunduliwa na jeshi la polisi!

Tume ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini imeanza kutumia mbinu mpya kudhibiti dawa hizo katika mipaka iliyopo hapa nchini ikiwemo mipaka ya Tunduma na Kasumulu katika mikoa ya Mbeya na Songwe.
Mkuu wa kitengo cha kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya hapa nchini, Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi Mihayo Misikela amesema mbinu hizo zimeanza kutolewa kwa wakuu wapelelezi wa jeshi la Polisi ngazi ya wilaya na mikoa ili kuwabaini wasafirishaji na waingizaji wa dawa za kulevya hapa nchini.
Wakati huohuo mwakilishi wa mkemia mkuu wa Serikali Bwana Aloyce Ngonyani amesema kuwa wametoa vifaa mbali mbali vya utambuzi wa awali wa dawa za kulevya kwaajili ya makundi ya dawa mbali mbali na utambuzi wa kemikali
Mipaka ya Kasumulu na Tunduma ndio mipaka maarufu inayosemekana inapitisha zaidi madawa ya kulevya.

Sunday, October 9, 2016

Anyofolewa Kiganja cha Mkono wa Kulia na kuuawa!

Mwalimu Israel Mlowasa (40) wa Shule ya Sekondari Nkuhungu katika Manispaa ya Dodoma, amekutwa ameuawa nyumbani kwake na kiganja chake cha mkono wa kulia kukatwa na kuondoka na wauaji hao.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi inasema kwamba mauaji hayo yamefanyika juzi maeneo ya Chang’ombe Extension katika Manispaa ya Dodoma.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Nkuhungu, Fidelis Kaishozi alisema mwalimu huyo alipotea tangu Oktoba 2, mwaka huu na taarifa kutolewa Polisi.

Imeelezwa kuwa maiti ya mwalimu huyo ilikutwa katika pagala la nyumba eneo la Nkuhungu.

Hakuna mtu aliyekamatwa kuhusu mauaji hayo, msako mkali unaendelea ili kubaini wahusika na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Dodoma kwa uchunguzi zaidi wa madaktari.

Chanzo: Mpekuzihuru

NECTA Kupigilia Panga la Mwisho Kwa Wenye Vyeti FEKI Kuanzia Kesho.....Watumishi Wote Kufuatwa Vituoni Kukaguliwa

Hatua ya Baraza la Mitihani nchini (Necta) kutoa ratiba ya kufanya uhakiki wa vyeti vya kidato cha nne, sita na ualimu kwa watumishi wote wa umma sasa ni wazi imezidi kupandisha joto kwa vigogo na watumishi mbalimbali ambao hawana sifa za kielimu kushika nafasi walizo nazo.

Katika taarifa yake ya sasa Baraza la Mitihani nchini, limetangaza kuwafuata katika maeneo yao ya kazi watumishi wote walioko katika mamlaka za mikoa, halmashauri na manispaa kwa ajili ya kufanya uhakiki wa vyeti vyao hivyo vya kitaaluma.

Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na  Edga Kasuga kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Baraza hilo kwenda kwa Makatibu tawala wa Mikoa, uhakiki utafanyika katika ofisi za Makatibu Tawala wa mikoa kuanzia Oktoba 10 hadi 14 mwaka huu, ingawa ratiba nyingine ya uhakiki imeonyesha zoezi hilo litafikia tamati Novemba 7 mwaka huu.

“Ili kufanikisha zoezi hilo Baraza limetaka kupata orodha (nakala- laini ya soft copy) ya watumishi wote wa umma waliopo katika Mkoa, Halmashauri na Manispaa.

“Nakala za vyeti vya kidato cha nne, cha sita na ualimu vya watumishi wote walioandikishwa na chumba cha kufanyia uhakiki,” inaeleza taarifa hiyo ya Baraza la Mitihani.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani, uhakiki huo utafanywa katika makundi matano katika mikoa tofauti tofauti.

Oktoba 10, mwaka huu kundi la kwanza litafanya uhakiki katika Mkoa wa Mtwara, kundi la pili Singida, kundi la tatu Rukwa, kundi la nne Katavi na kundi la tano litakuwa Geita.

Oktoba 17 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Lindi, la pili Manyara la tatu Songwe, la nne Kigoma na la tano litakuwa Mwanza.

Oktoba 24 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Morogoro, la pili Arusha, la tatu Mbeya, la nne Tabora na la tano Mara.

Oktoba 31 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Pwani, la pili Kilimanjaro, tatu Ruvuma, la nne Shinyanga na la tano Simiyu.

Novemba 7 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Dar es Salaam, la pili Tanga, la tatu Njombe, la nne Dodoma na la tano Iringa.

Saturday, October 8, 2016

Hapa ni habari kamili ya kifo cha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Dodoma

Kuna taarifa za majonzi za kifo cha Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake Tanzania UWT Mkoa wa Dododma ambapo chanzo cha kifo hicho kilikua kinaleta utata.

Mashuhuda  wa ajali wamesema alikufa kutokana na kushindwa kupewa msaada kwa haraka.

Walisema baada ya ajali walisikia sauti za watu wakilia kuomba msaada lakini ilichukua muda wa sasa tatu ndipo walipopata msaada wa kuokolewa kutokana na ukosefu wa vifaa vya uokoaji.

Juzi katika eneo la Emmaus mkoani hapa ilitokea ajali ya gari la Toyota Noah na lori ambayo ilichukua maisha ya Mwenyekiti huyo na watu wengine watatu kujeruhiwa. 

Mmoja wa mashuhuda hao Amri Juma alisema alisikia sauti za wanawake wakiomba msaada ili waweze kuokolewa.

“Ni jambo la kusikitisha kuona zaidi ya saa tatu hakuna vifaa vya uokoaji vilivyokuwa vimefika kwa ajili ya uokoaji, ajali ilitokea saa nane mchana lakini mpaka saa 11 jioni ndio watu wanakuja kutolewa.

‘’‘Breakdown moja ilipofika ilishindwa kunyanyua lori, ilipofika ya pili ilishindwa, hali inayoonesha kuna uhaba wa vifaa hivyo mamlaka husika zijipange kuwa na vifaa vya uokoaji."

 Juma alisema Dodoma imeanza kuandaliwa kuwa makao makuu ya nchi hivyo wakati umefika wa kuanza kujengewa uwezo wa kuwa na vifaa vya kisasa vya uokoaji. 

Katibu wa UWT Mkoa wa Dodoma, Kaundime Kasase, akizungumzia kifo hicho alisema;

“imeniuma sana na bado inaniuma, sina hata la kusema kwani nimefanya naye kazi kwa ukaribu, alikuwa mtu anayependa viongozi wake wote."

Mtoto aliyekuwa ndani ya gari hilo, Dearest Mabuba (8) alisema;“Tulikuwa tumetoka kwenye birthday (siku ya kuzaliwa) yangu ndipo gari likapata ajali, mama yangu Annastazia Amandus ambaye alikuwa akiendesha gari hilo akaumia kichwani na dada akachanika kwenye kiwiko,” alisema.

Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jaffari Mwanyemba alisema wamempoteza mtu muhimu.

“Alikuwa akijichanganya kila mahali, tumepoteza mtu muhimu tuige mazuri yake”. 

Mbunge wa Viti Maalumu na Mwenyekiti mstaafu wa UWT Mkoa wa Dodoma, Fatma Tawfiq alisema;

“Mwenyezi Mungu ndiye alikuwa akifahamu siri hii. “Ni jambo la kushtukiza sana tumuombee Mungu amuweke mahali pema peponi,”alisema.

Hata hivyo kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Dodoma, Marson Mwakyoma alisema walifika eneo la tukio dakika 10 baada ya ajali hiyo kutokea.

“Si lazima askari avae sare tulifika mapema na vikosi vingine vya uokoaji vilikuja kwa wakati, nadhani kitu muhimu kinachotakiwa kufanyika ni kuimarisha vifaa vya uokoaji,” alisema.

Chanzo | Mpekuzi

Ofisi Ya Makao Makuu Ya Hifadhi Ya Serengeti Yateketea Kwa Moto Leo Jumamosi

Leo Jumamosi Oktoba 8, 2016 Mkoani Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kumetokea janga la moto.

Taarifa kutoka Hifadhi za taifa Tanzania zinasema hivi:-
Ofisi ya makao makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti yaliyoko Fort Ikoma wilayani Serengeti mkoani Mara iemeteketea kwa moto leo Jumamosi tarehe 8, oktoba 2016.

Moto huo ulianzia katika ofisi ya tiba ya wanyamapori na kusambaa katika ofisi nyingine.

Hadi sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana na taarifa kamili itatolewa mara baada ya uchunguzi kukamilika ikiwa ni pamoja na kujua hasara kamili iliyotokana na moto huo.

Bodi ya Mikopo (HESLB ) Yasitisha Mikopo Ya Walimu Wanafunzi Waliompiga Mwanafunzi Mbeya

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inautaarifu umma kuwa imesitisha mikopo ya elimu ya juu iliyokuwa ikitolewa kwa walimu-wanafunzi wanne waliosimamishwa masomo kwa kuhusika katika tukio la kumshambulia na kumuumiza mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya. Walimu hao walikuwa katika mafunzo ya vitendo.

1. Frank Msigwa - Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)

2. John Deo- Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)

3. Evance Sanga - Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)

4. Sante Gwamaka - Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)

Kwa utovu huo wa nidhamu, wanafunzi hao wamesimamishwa masomo na mamlaka husika kwa hiyo wamepoteza sifa za kuendelea kupokea mikopo. 

Mikataba inayosainiwa na wanufaika wa mikopo inawataka wanufaika kuzingatia masharti kadhaa ikiwa ni pamoja na nidhamu na kufuata sheria na taratibu za vyuo na mamlaka halali.

Aidha, kwa mujibu wa taratibu za kukopeshwa, wanafunzi hawa watatakiwa kuanza kurejesha kiasi walichokopeshwa mara moja.

Bodi ya Mikopo inawakumbusha wanufaika wanaoendelea masomo kuzingatia masharti ya ukopeshwaji na kuheshimu sheria, kanuni taratibu na kuwa mfano mwema katika jamii. Mikopo na ruzuku zinazotolewa na Serikali ni kwa ajili ya kuwaandaa kuwa raia wema, waadilifu, na wachapa kazi ili kujenga uchumi imara na ustawi kwa wote.

Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru
Mkurugenzi Mtendaji

Ijumaa, Oktoba 7, 2016