Showing posts with label Habari za Elimu. Show all posts
Showing posts with label Habari za Elimu. Show all posts

Wednesday, October 12, 2016

Mwalimu aliyemtukana mwanafunzi wa kidato cha sita Iringa, Mahakama imetoa maamuzi!


Ikiwa matukio ya unyanyasaji mashuleni yakiendelea kutokea, Mahakama ya Mwanzo Iringa  Mjini imemuachia huru mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kiwele baada ya kukosa ushahidi wa kumtia hatiani katika kesi ya  kumtukana mwanafunzi.
Mwalimu huyo, Elizabeth Maliga (32) ameshtakiwa kwa madai ya kumtukana mwanafunzi huyo wa kidato cha sita, Rehema Mwakatobe na mama yake.
Amedaiwa kufanya kosa hilo wakati akimsainia Rehema barua ya kumuita mama yake kwenda shuleni hapo kusikiliza kosa la kuchelewa shuleni.
Hukumu hiyo imetolewa wakati Taifa likiwa kwenye mjadala mkubwa baada ya picha za video zilizosambaa mitandaoni kuonyesha kundi la walimu wa Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya likimshambulia mwanafunzi Sestian Chikungu.
Tayari Serikali imeshatangaza kuwafukuza chuo walimu hao na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi.
Akisoma hukumu ya kesi hiyo iliyochukua takriban dakika 45, Hakimu wa Mahakama hiyo,  Abdallah Kutvai alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuishawishi mahakama kumtia hatiani mshtakiwa huyo.
“Jukumu la kuthibitisha kosa ni la upande wa mashtaka. Hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha tano cha Sheria ya Ushahidi ya Mahakama ya Mwanzo iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
“Mashahidi wa upande wa mashtaka wametofuatiana tarehe za kutendwa kosa hilo. Shahidi namba moja ambaye ni mlalamikaji anasema kosa limetendeka Septemba 13, mwaka huu kwenye kikao cha kujadili mwenendo wa utekelezaji wa adhabu zilizotolewa na walimu kwa wanafunzi shuleni hapo,”alisema Hakimu Kutvai.
Amefafanua kuwa shahidi namba mbili alishindwa kubainisha siku ya tukio na kutaja tarehe tatu tofauti, ambazo ni Septemba 13, 14 na 15, siku ambayo mwanafunzi huyo alipewa barua ya kurudishwa nyumbani kwao Dar es Salaam kumfuata mzazi.

Monday, October 10, 2016

Kinachoendelea kuhusu Mwalimu Frank Msigwa na utata wa akaunti yake ya Instagram!

Baada ya kufukuzwa Chuo kwa hatua yao ya kushiriki kitendo cha kumpiga mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya kutwa ya sekondari mkoani Mbeya (Mbeya Day), Mwanafunzi Sebastian Chingulu tamko lililotolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako , Mwalimu Frank Msigwa  hatimaye ameibuka na kuomba msamaha kwa Watanzania.Frank Msigwa kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, (frank_msigwa_) ambayo hadi leo Oktoba 10.2016 akaunti hiyo imeweza kupata Followers 741 na Following  ikifikia 2065,   huku akiwa ameposti mara m ili tu ikiwemo post yake ya jana Oktoba 9 juu ya tamko lake hilo la kuomba msamaha na leo kupost tamko la kusikitishwa kwake kwa Watanzania walivyopokea msamaha wake huo. (Angalia picha).Watu mbalimbali wamekuwa wakichukulia tofauti msamaha wake huo na hata wengine wakiubeza kuwa ni akaunti ‘feki’ ya Mwalimu huyo Mwanafunzi Frank  Msigwa.Mbali na kuona suala hilo la msamaha kwa kijana huyo kupitia mitandao ya kijamii watu mbalimbali wameeleza kuwa alipaswa kwenda kwenye vituo vya radio na TV kuomba msamaha huo huku wengine wakimtaka aende kwa wazazi wa mtoto aliyepigwa ndio wataweza kumsamehe.Kwa hali hiyo hadi sasa bado Frank Msigwa anazua maswali mengi kwa wananchi kama ni kauli yakke kutoka kinywa chake ama ni mtu ameamua kufanya hivyo kwa niaba ya Msigwa?..

Huu ndio ujumbe unaodaiwa ni wa mwalimu Frank Msigwa....frank msigwa