Showing posts with label Habari za kimataifa. Show all posts
Showing posts with label Habari za kimataifa. Show all posts

Monday, January 30, 2017

Kutana na Mfungwa aliyefaulu Shule Gerezani na sasa atakwenda chuo kikuu London

Inatokea kwenye gereza la Naivasha Kenya ambapo Mfungwa Michael Kahiga ni miongoni mwa Wafungwa wachache watakaojiunga na chuo kikuu kutokana na jitihada zake za kujisomea kwa bidii chini ya Mwalimu wake pia ambaye pia ni Mfungwa wa kifungo cha maisha.
Kwenye gereza hilo la Naivasha kuna Liblary ambayo ina vitabu mbalimbali ambapo Michael anasema pamoja na yeye kufaulu kwenda chuo kikuu, kwenye kusoma kwake akiwa gerezani bado hakuwa na Waalimu ambao wamekidhi vigezo.
Michael anatumikia kifungo cha miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya wizi ambapo baada ya kumaliza kifungo chake, atajiunga na chuo kikuu cha London Uingereza ambacho kimempa nafasi ya kusoma bure kwenye chuo hicho baada ya kufaulu vizuri kwenye mtihani wa kitaifa gerezani.
Kwa mujibu wa K 24 Kenya, kwenye mtihani aliofaulu Michael ni Wanafunzi 141 walipata A ambapo Michael mwenyewe alipata C+, unaweza kumtazama kwenye hii video hapa chini.

Friday, January 27, 2017

Rais Adam Barrow arudi Gambia kuliongoza taifa lake


Rais mpya wa Gambia Adama Barrow, amewasili nchini humo kuchukua hatamu za uongozi, kufuatia kuondoka madarakani kwa rais wa mda mrefu Yahya Jammeh
Barrow aliapishwa wiki iliyopita nchini Senegal wakati viongozi wa kieneo walipokuwa wakimshawishi Jammeh kuondoka madarakani.
Maelfu ya watu walifurika katika barabara za mji mkuu wa Gambia Banjul kumlaki rais huyo mpya.
Taarifa zinasema Barrow atakaa katika makaazi yake wakati ukaguzi ukifanywa katika ikulu kutambua hatari yoyote kufuatia kuondoka kwa Yahya Jammeh kwenda uhamishoni Guinea ya Ikweta.
Maelfu kadhaa ya wanajeshi wa mataifa ya Afrika magharibi wanasalia Gambia wakati kukiwa na taarifa kuwa wafuasi waovu wa Jammeh wamo miongoni mwa vikosi vya usalama nchini.

Tuesday, October 11, 2016

Ujerumani wamefanya jambo kwaajili ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere

Leo October 11 2016 BBC wameripoti taarifa ya Chancellor  wa Ujerumani Angela Merkel kuzindua jumba jipya la makao makuu ya Umoja wa Afrika ambalo limepewa jina la baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuelekea siku ya kumbukumbu tarehe 14.
Jumba hilo ambalo jina lake kamili ni Jumba la Amani na Usalama la Julius Nyererelimejengwa kwa ufadhili kutoka Ujerumani, litakuwa makao ya idara ya Amani na Usalama ya AU na litatumiwa pia na maafisa wa kutoa tahadhari ya mapema kuhusu mizozo barani pamoja na kuratibu juhudi za kulinda amani za AU.Ujenzi wa jumba hilo, ambalo ukubwa wake wa sakafu ni mita 13,500 mraba na linaweza kutumiwa na wafanyakazi 360, uligharimu euro milioni 27. Jumba hilo ofisi za kufanyia kazi, vyumba vya mikutano vya kutumiwa na Baraza la Amani na Usalama, chumba cha kuratibia shughuli, maktaba na vyumba vya shughuli za pembeni.Mwalimu Nyerere, ambaye alikuwa rais wa Tanzania hadi 1985, alikuwa mmoja wa viongozi waanzilishi wa Muungano wa Nchi za Afrika (OAU) ambao sasa ni Umoja wa Afrika (AU). Alishiriki sana katika jitihada za kuendeleza bara la Afrika na kusaidia mataifa ambayo hayakuwa yamepata uhuru kujipatia uhuru wake.

Monday, October 10, 2016

Mjadala wa urais Marekani: Trump amshambulia Clinton

Hillary Clinton na Donald Trump katika mjadala wa Urais

Wakati Donald Trump na Hillary Clinton walipokwea jukwaani St Louis kwa mjadala wa pili kati ya mitatu iliyopangwa, hakupeana salamu kwa mikono , jambo lililodhihirisha chuki ambayo ingeendelea katika kipindi kizima cha mjadala huo.Donald Trump ametangualia kwa kutetea matusi aliyotoa kuhusu kuwagusa wanawake katika sehemu za siri kwa kumshambulia Hillary Clinton na mumewe.Mgombea huyo wa chama cha Republican, amekana kamwe hajawanyanyasa wanawake kingono, lakini akageuza hasira kwa aliyekuwa rais wa Marekani Bill Clinton katika majibizano makali kwenye mjadala huo"Hakuna mtu katika historia ya siasa ambaye amewanyanyasa wanawake kiasi hicho," alisema.Hillary Clinton alikataa kujibu tuhuma hizo dhidi ya mumewe.Matamshi ya bwana Trump dhidi ya failia ya Clintons yalijiri baada ya muendesha mjadala Anderson Cooper kumuuliza kuhusu kanda ya video ya mwaka 2005 iliyosambazwa katika vyombo vya habari Ijumaa iliyomfichua Trump akijigamba kuhusu kuwagusa wanawake katika sehemu zao za siri.Lakini alipoendelea kuulizwa kuhusu iwapo alimnyanyasa kingono mwanamke yoyote, alikana kufanya hivyo na badala yake akamulika tuhuma zilizomuandamana Bill Clinton katika siku za nyuma.Hakuna mashtaka ya uhalifu yaliowasilishwa dhidi ya Bwana Clinton katika tuhuma zozote z unyanyasaji wa kingono.Wagombea hao wawili bila walizozana kuhusu mzozo wa Syria, Uchokozi wa Urusi, na hatua ya bwana Trump kukata kutangaza malipo yake ya kodi na mpango wake wa ukaguzi mkali kwa wahamiaji wanaowasili kutoka mataifa yanayohusishwana ugaidi.Hatimaye mjadala ulikamilika wakati mwanamume mmoja kutoka umati uliokusanyika kufuatilia mjadala huo, alipowauliza wagombea hao wawili kusema kitu kimoja kizuri kumhusu mwenzake.Mgombea wa chama cha Democrat Hillary Clinton akasema watoto wake Trump wanamdhihirisha ni mtu wa aina gani.Naye Trump akamtaja mpinzani wake kuwa "mpiganaji" asiye kata tamaa.

Sunday, October 9, 2016

Hii ya China kushinda tuzo ya kutambua mvinyo duniani kwa kuonja imekaaje!

China imeshinda shindano la kutambua mivinyo kupitia kuonja
Kundi moja la wataalam nchini China limeshinda tuzo la shindano la kuonja mvinyo nchini Ufaransa.
Watalaam hao walitambua mivinyo waliopewa huku wakiwa wamefunikwa uso,wakibainisha asili, aina ya zabibu zilizotumika na mwaka mivinyo hiyo iliotengezwa.
Waandalizi wa shindano hilo waliwataja wataalam hao wa China kuwa mabingwa katika ulimwengu wa mvinyo.
Waliyashinda mataifa mengine 20,ikiwemo washindi wa awali Ubelgiji na Uhispania.
Huku mapato yakiongezeka nchini China,taifa hilo linaongoza katika utengezaji na utumiaji wa mvinyo duniani.

John McCain na Condoleezza Rice wajiondoa kumuunga mkono Trump kwenye uchaguzi huko Marekani

trump
Viongozi zaidi wa juu wa chama cha Republican, wamejiondoa kumuunga mkono mgombea urais wa Marekani wa chama hicho, Donald Trump baada ya maneno ya dharau aliyoyasema dhidi ya wanawake miaka 10 iliyopita kuvuja.
Zaidi ya viongozi 10 wa chama hicho wamesema hawatampigia kura Trump tangu kauli hiyo isambae kuanzia Ijumaaa. Trump anasema katu hatojiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho na kwamba hatowaangusha wafuasi wake.
Amekuwa kwenye kiti moto tangu video ya mwaka 2005 kuvuja akisikika akiongea kuhusu kuwabusu wanawake na kuwashika sehemu zao za siri.
Viongozi wa Republican waliojiondoa kumuunga mkono ni pamoja na mgombea wa zamani wa kiti hicho John McCain na waziri wa zamani mambo ya nje, Condoleezza Rice.
McCain amesema kauli ya Trump inafanya ishindikane kumuunga mkono kwenye harakati zake. Naye Bi, Rice amesema: “Enough! Donald Trump should not be President. He should withdraw.”
Seneta wa New Hampshire, Kelly Ayotte amesema kwenye maelezo yake: I cannot and will not support a candidate for president who brags about degrading and assaulting women.”
Mke wa Trump, Melania naye alitoa maelezo Jumamosi akisema: The words my husband used are unacceptable and offensive to me.” Hata hivyo alimtetea akidai kuwa mumewe ana moyo na fikira za kiongozi.