Saturday, October 8, 2016

Kesi ya Neymar sasa ni mahakamani!

Wakati Juzi Neymar akipiga Bao lake la 300 katika maisha yake ya Soka wakati Nchi yake Brazil ikiitwanga Bolivia 5-0 kwenye Mechi ya Kanda ya Marekani ya Kusini kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018, huko Spain Waendesha Mashitaka wameitaka Mahakama kumfungulia Mchezaji huyo Mashitaka ya Udanganyifu na Rushwa kuhusu Uhamisho wake wa kutoka Klabu ya Brazil Santos kwenda Barcelona wa Mwaka 2013.
Mbali ya Neymar, wengine ambao wanakabiliwa na Mashitaka hayo ni Baba yake Mzazi pamoja na Rais wa Barcelona, Sandro Rosell, na Rais wa Klabu ya Santos, Odilo Rodrigues.
Mashitaka hayo yanahusishwa na Udanganyifu na Rushwa kwa madai kuwa Fedha halisi za Uhamisho wa Neymar zilifichwa ili kuidhulumu Kampuni ya Brazil, DIS, ambayo pia ilikuwa ikimiliki Haki za Kibiashara za Neymar.

IKUMBUKWE:
-Mwaka 2013, Barcelona walitangaza kuwa Ada ya Uhamisho ya Neymar kutoka Santos ya Brazil kwenda Barcelona ilikuwa Euro Milioni 57.1 huku Euro Milioni 40 akilipwa Neymar na Familia yake na Santos kupokea Euro Milioni 17.1 ambapo kati ya hizo Euro Milioni 6.8 zililipwa kwa Kampuni ya DIS iliyomiliki Asilimia 40 ya Haki za Kibiashara za Neymar
-Madai yakaibuka kuwa Ada halisi ni Euro Milioni 83.

Awali Mahakama huko Spain chini ya Jaji Jose de la Mata iliitupa Kesi hiyo ikidai ni ya Madai na si Uhalifu lakini sasa imeamuliwa ifufuliwe tena baada ya Waendesha Mashitaka kukata Rufaa na kushinda.
Neymar, ambae alipasuliwa Usoni kwenye Mechi ya Jana na Bolivia na kutolewa nje na kubadilishwa, ameruhusiwa kurejea Spain kutoka Kambi ya Brazil kwa sababu haruhusiwi kucheza Mechi yao ya Jumatano Ugenini na Venezuela baada ya kupata Kadi ya Njano iliyompa Kifungo cha Mechi Moja.

No comments:

Post a Comment