Friday, October 14, 2016
Aliyetobolewa macho aongezewa misaada zaidi
Nadhani unakumbuka vizuri ishu ya jamaa mmoja jijini Dar es Salaam Said Ally alivyoeleza namna alivyofanyiwa ukatili na kutobolewa macho yake mawili mbele ya umati wa watu katika eneo la Buguruni, watu wengi wamejitolea kwa hali na mali kumsaidia ili aweze kumudu gharama za maisha.
Mwinyi asema ana wasiwasi na Tanzania tuliyopo
Ikiwa Tanzania leo inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 17 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amesema ana wasiwasi na Taifa la sasa kwani halina uadilifu, aliotujengea Mwalimu Nyerere.Mwinyi aliyerithi mikoba ya urais kutoka kwa Mwalimu Nyerere mwaka 1985, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mdahalo wa kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na kuzindua kitabu cha ‘Selective works of Mwalimu Nyerere’, kilichotafsiriwa na wasomi kutoka China.
Mdahalo huo uliandaliwa na Taasisi ya Uongozi ikishirikiana na Ubalozi wa China na Asasi ya Urafiki kati ya Tanzania na China. Mwalimu Nyerere aliyeitawala Tanzania kwa takribani miaka 24, alifariki dunia Oktoba 14, 1999 kwenye Hospitali ya St Thomas jijini London nchini Uingereza ambako alikuwa akitibiwa maradhi ya saratani ya damu.
Aliiongoza Tanzania kwa uadilifu mkubwa akisimamia misingi ya haki, umoja, mshikamano, kupiga vita rushwa, kusisitiza kujitegemea na uzalendo kwa nchi.
“Kazi za kawaida kweli zinafanywa na zinaendelea, lakini sina uhakika hata kidogo kama uadilifu aliotuachia Mwalimu bado tunao, sijui nani wa kulaumiwa,” alisema Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa. Alisema kwa namna ambavyo mambo yanakwenda, ni kiashiria tosha kuwa nchi haina uadilifu tena.
“Mambo yanavyokwenda kama gari lililo katika usukani,” alieleza Mwinyi na kuongeza kuwa kuna kila sababu ya kutafakari hali ilivyo sasa ikilinganishwa na ile ambayo iliachwa na Baba wa Taifa miaka hiyo 17 toka kufa kwake.
Alisema nafasi hiyo ya mazungumzo katika mdahalo, inawapasa kukaa kutafakari namna ya kurudisha nchi kwenye reli ambayo iliachwa na Mwalimu Nyerere ambaye ndiye muasisi wa taifa hili katika misingi ya uongozi.
“Tuna utajiri wa machoni, lakini ndiyo aliyokusudia Mwalimu? Alitufundisha tuwe matajiri wa vitu au matajiri wa moyo? Tujali vitu au tujali utu?” Alihoji Rais huyo mstaafu.
Isikupite hii ya diwani wa Chadema kunaswa na dawa za kulevya pamoja na bunduki
Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa linamshikilia Diwani wa kata ya Izira, Paschael Silimba (Chadema) baada ya kumkamata akiwa na dawa za kulevya aina ya bangi na bunduki moja aina ya gobole.Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, George Kyando amesema kuwa jeshi hilo lilimkamata Kyando katika eneo la soko kuu ambalo hufanyia biashara yake ya kuuza mifuko ya salfeti, baada ya kupata taarifa na kuamua kumfuatilia.Alisema kuwa baada ya kumpekua katika vifurushi vya bidhaa hiyo anayoiuza kwa kushirikiana na mkewe, walibaini uwepo wa bangi kiasi cha robo kilo.“Baada ya kufanya upekuzi kwenye duka la diwani huyo, tumefanikiwa kukamata bangi kiasi cha robo kilo. Ni bangi kavu ambayo imeshaandaliwa tayari kwa ajili ya kufanya packing na kuuzwa,” alisema Kamanda Kyando.Akizungumzia silaha aina ya gobole waliyoikuta nyumbani kwa diwani huyo anayodaiwa kuimiliki kinyume cha sheria, alisema ingawa ni silaha ya kizamani ina nguvu ya kuua tembo.“Silaha hii ina nguvu sana, ina uwezo wa kuua tembo na ni hatari sana akipigwa binadamu kwa silaha hii. Kwahiyo msiione hapa mkaidharau, ina nguvu sana,” aliongeza.Kamanda Kyando aliwataka viongozi wote waliopewa dhamana na wananchi kutotumia nyadhifa zao kufanya uhalifu. Alitoa wito wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kufichua uhalifu bila kujali waliofanya uhalifu huo.
Mbowe aahidi kuipeleka mahakamani serikali ya awamu ta tano
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema atapeleka Serikaliya Awamu ya Tano mahakamani ili chombo hicho cha haki kitoe tafsiri ya vitendo vya ukandamizaji wa demokrasia vinavyofanywa na viongozi wa Serikali hasa Mkoani Arusha.
Mbowe ameyasema hayo alipokuwa akilaani kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, kuwasweka selo madiwani wanne wa chama hicho akisema kuwa hiyo ni ishara ya kwamba utawala wa awamu ya tano hauheshimu sheria.
“Nimewaagiza wanasheria wangu kwenda mahakamani ili kupata tafsiri sahihi kuhusu vitendo hivyo,” amesema.
Ameongeza kuwa viongozi hao wamekuwa wakifanya vitendo vya udhalilishaji kwa baadhi ya wabunge, madiwani, mameya na wenyeviti wa halmashauri kinyume na sheria.
“Nawashangaa sana Wakuu wa Mikoa na Wilaya wamekuwa wakiwadhalilisha wawakilishi wa wananchi ilhali wao wakiwa ni waajiriwa ambao hawajaomba kura kwa wananchi. Jambo hili limeanza mwaka huu, nah ii ni nafasi mbaya sana kwa Rais Magufuli kuchagua makada badala ya watumishi,” amefunguka Mbowe.
Kuhusu ishu ya makontena 100 kupitishwa Bandarini bila kukaguliwa, Waziri mwaijage katoa muda mchache wa wahusika kujisalimisha
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage ametoa siku nne kwa wafanyabiashara waliopitisha makontena 100 bandarini bila kukaguliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), wakatoe taarifa katika shirika.Mwijage alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupata taarifa kuwepo kwa makontena 100, yaliyotolewa bandarini kwa siku zilizopita bila kukaguliwa na TBS.“Nawataka wafanyabiashara wote waliochukua kontena hizo, wajisalimishe haraka TBS kabla ya kufika Jumanne ili wakaguliwe. Najua kuanzia kesho (leo) ni mapumziko, lakini TBS itaweka dawati la kuwasikiliza mpaka Jumatatu na ikifika Jumanne hatua zitachukuliwa kwa wahusika wote,” amesema Mwijage.Alisema wafanyabiashara ambao hawatajisalimisha baada ya kumalizika kwa siku hizo, hatua stahiki zitachukuliwa ikiwemo kulipa faini ya asilimia 15.Aidha, alisema kwa mawakala wa forodha wote, waliohusika kutoa kontena hizo wizara yake itawasiliana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ili kuona hatua za kuchukua kwa kuwa serikali haiwezi kukubali mchezo huo.“Tayari tulishafunga michezo ya namna hii na tumeanza maisha mapya kwa hiyo mawakala na wote mliohusika kutoa kontena hizo sababu hazijafika mbali tunaomba mtueleze zilipo ili tukazikague,” aliongeza.Pia alisema kontena hizo zilipaswa kukaguliwa na TBS, lakini baada ya tukio hilo kontena hizo zitakaguliwa na shirika hilo wakishirikiana na Tume ya Ushindani Tanzania (FCC). Aidha, amewaagiza TBS na FCC wafuatilie watu wao na kuziona bidhaa hizo, kwani watakaoshindwa hawatapewa cheti cha ubora bila kuona bidhaa na kukaguliwa.“Sisi hatutaki mje mtueleze ni mzigo kiasi gani ili tupige penati hapana tunataka hilo kontena mlione na hiyo bidhaa muione na mkague,”aliongeza waziri huyo.Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk Egid Mubofu alisema ni vyema wafanyabiashara hao wakafuata maagizo hayo na kujitokeza kukaguliwa ilikuepuka faini hiyo ya asilimia 15. Alisema upitishaji wa bidhaa bila kukaguliwa na shirika hilo unaweza kuleta madhara makubwa kwa watumiaji ambao hawajui kama bidhaa yako imekaguliwa ubora.“Najua wafanyabiashara wengine watasema hatuendi kukaguliwa sababu hataitumia bidhaa hiyo, lakini anasahau kama anaweza siku moja na yeye akatumia bidhaa hiyo ambayo haijakaguliwa ni vyema wakawa wazalendo na kufuata maagizo waliyopewa,” alisema Mubofu.TBS imeanzisha utaratibu mpya wa kulipisha faini mizigo inayoingia hapa nchini, ambayo haikukaguliwa wakati iko nchini China. Faini ni asilimia 15 ya thamani ya mzigo ulioingia.
Thursday, October 13, 2016
Kurasa za Magazeti: Leo Ijumaa Oktoba 14, 2016
Kuna habari mbali mbali zimeandikwa leo Ijumaa Oktoba 14, 2016 kwenye magazeti ya Tanzania na nje ya Tanzania. Hapa tuangalie kurasa za mbele na nyuma za magazeti ya leo Tanzania yameandika habari gani kisha tujadili pale chini kwa kuandika maoni yetu.
Davido ft Tinashe - How Long | Listen and Download Mp3
Most anticipated video of the year off the SON OF MERCY EP from Davido is finally Out, This features international artist Tinashe .Watch!!
New Music Audio: Timaya ft Iyaz - How Many Times | Listen and Download Mp3
Timaya is here with a new Bang , this new record from the Egberi Papa just surfaced online.This new sound which is a leak is titled “How Many Times” and Iyaz is featured on this one with production credit from Kenny Wonder.
Wednesday, October 12, 2016
Kurasa za Magazeti: Leo Oktoba 13, 2016
Subscribe to:
Posts (Atom)