Tuesday, July 26, 2016

Taarifa ya ajali ya basi la Uda usiku wa tarehe 26 Julai, 2016


Ajali imetokea usiku wa tarehe 26 kati ya treni na basi la Uda linalofanya safari zake kati ya Kariakoo na Mbagala jijini Dar es Salaam na kuua mtu mmoja na wengine zaidi ya 45 kujeruhiwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Ernest Matiku amesema majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.
Hata hivyo, hakuweza kumtaja jina mtu huyo aliyefariki dunia.
“Ni kweli ajali imetokea kuna kifo cha mtu mmoja na watu wengi wameumia sana na hivi ninavyozungumza na wewe naelekea Muhimbili,” amesema Kaimu kamanda huyo.

No comments:

Post a Comment