Tuesday, July 26, 2016

Taarifa kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa juu ya mauaji ya Daudi Mwangosi.

Mahakama kuu kanda maalumu ya Iringa leo imesendelea na kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha cha Channel Ten mkoani Iringa, Daud Mwangosi, inayomkabili askari wa kikosi cha kutuliza ghasia’FFU’, Pasifius Simon.
Hukumu ya kesi hiyo awali ilipangwa kutolewa July 21 mwaka huu, iliahirishwa hadi leo kutokana na jaji anayesikiliza kesi hiyo kuwa nje ya mkoa kikazi.
Leo July 25 2016 taarifa iliyoripotiwa na kituo cha ITV muda huu ni kwamba mahakama kuu Iringa imemtia hatiani kwa kuua bila kukusudia askari huyo na hivyo hukumu rasmi itatolewa siku ya jumatano.

No comments:

Post a Comment