Sunday, July 24, 2016

Diva amuongeza Chemical na rappers wengine wanne kwenye remix ya Baby Boy


Mtangazaji wa Clouds FM, Diva The Bawse amemuongeza Chemical na rappers wengine wanne kwenye remix ya wimbo wake Baby Boy.
remix hiyo ndio itatumika kama wimbo official kwaajili ya redio na pia kuja na video yake. Version ya kwanza iliyokuwa na Mr Blue na Bill Nas ilikuwa ni kwaajili ya mtandaoni peke yake.
“Chemical atafungua verse ya kwanza this time, yeye ndio ataanza,” amesema Diva.
“The remix is way better, so billnass atasikika pia, Mr Blue and wengine ambao ni wakubwa but surprise,” ameongeza.
Pia Diva amesema amemaliza tofauti yake na Bill Nas.
“We good right now.. aliapologize .. guess magazeti nayo wachonganishi, so we agreed he is gonna kill with a killer verse.”

No comments:

Post a Comment