Sunday, July 24, 2016

FA imemtangaza kocha mpya wa England leo July 22 2016

England ni moja ya mataifa yenye bahati mbaya sana kwenye tasnia ya soka. Ni taifa ambalo linatumia nguvu nyingi sana kujitangaza lakini pengine linaongoza kwa matokeo mabaya miongoni mwa mataifa yenye nguvu katika soka ulimwenguni.
Hivi karibuni baada katika Michuano ya Euro, ambapo England walitolewa na timu ambayo naweza kusema ilikuwa ‘underdog’ kuliko timu zote kwenye michuano ile, timu ambayo ina idadi ya watu wasiozidi 330,000 na ambayo ilikuwa ikishiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza ukilinganisha na England ambao ni magwiji.
Baada ya matokeo hayo aliyekuwa kocha wa timu hiyo Roy Hodgson aliamua kujiuzulu kutokana na fedheha aliyokumbana nayo na nafasi kuwa wazi kwa muda.
FA walitangaza kuanza mchakato wa kutafuta mrithi wa Hodgson na makocha mbalimbali kuwekwa kwenye orodha hiyo.
Jurgen Klinsmann, Harry Redknapp, Eddie Howe, Glenn Hoddle na Arsene Wenger na Sam Allardyce wote walihusishwa kuchukua mikoba hiyo. Kwa namna yoyote ile Arsene Wenger asingeweza kukubakli kutokana na kuwa bado na mkataba wa Arsenal, lakini wengine wote walikuwa na nafasi.
Kitu kimoja ambacho England kwa miaka mingi wamekikosa ni kukosa ubora wa makocha kwenye kwenye taifa lao. Wana utitiri wa makocha lakini wasio na uwezo wa kufanya maajabu yoyote makubwa.
Baada ya mchakato wote kupitia na mchujo kupita, alyekuwa kocha wa Sundeland Sam Allardyce amefanikiwa kutwaa jukumu hilo.
Kuwa kocha wa taifa kama England ni moja na majukumu mazito kwa kocha yeyote kuyakubakli duniani kama ilivyo kwa mataifa kama Brazil, Ufaransa nk.
Kila maoni unayotoa kwenye mkutano na wanahabari, mabadiliko kwenye kikosi, uchaguzi wa wachezaji kwenye timu, nani wa kuchaguliwa na nani wa kuachwa…mambo yote haya yanapewa kipaumbele kikubwa na vyombo vya habari nchini humo.
Wakati huo huo jamii ya watu wa England wana matarajio makubwa kupambana kwenye kila aina ya michuano mikubwa licha ya kwamba timu yao imekuwa haina matokeo mazuri sana kwenye mashindano mbalimbali zaidi ya yale ya Kombe la Dunia mwaka 1966, ambapo walifika nusu fainali na Euro 1996 ambapo pia walifika nusu fainali, na michuano yote hiyo ilifanyika katika ardhi yao ya nyumbani.
Kuna makocha ambao wameshindwa kabisa kuendana na presha ya timu hiyo. Makocha hao ni pamoja na Roy Hodgson na Steve McClaren
Pengine na Fabio Capello, lakini huyu alijitahidi kwa nafasi yake.
Allardyce anaenda kukutana na mtihani mkubwa mno ambao umewashinda wenzake wengi katika timu hiyo.
Kuna hili la makocha wengi kuita wachezaji wengi wenye majina makubwa hata kama hawapo kwenye kiwango bora. Hilo ndilo limekuwa liiwatafuna makocha wengi walipokea kibarua cha England. Kwa mfano kwenye Michuano ya Euro mwaka huu, Hodgson alimwita Wilshare ambaye hakuwa na muda mwingi wa kucheza kutokana na kuuguza majeraha na kumwacha kiungo aliyecheza kwa mafanikio na kuchangia kuipa Leicester ubingwa wa EPL 2015/16 Daniel Drinkwater.
Majina mengine makubwa ambayo yamekuwa yakiogopwa na pamoja na Joe Hart, Wayne Rooney na Raheem Sterling.
Allardyce kwa namna ambavyo amezifundisha timu kadhaa kwenye ngazi ya klabu amekuwa na utofauti mkubwa.
Licha ya muda wake mwingi katika maisha yake ya ukocha kupewa timu za viwango ama vya kati au vya mwisho (middle tabke teams), lakini Allardyce hajawahi kuishusha timu daraja na mara zote amekuwa akiziacha timu kwenye nafasi nzuri tu ambazo si hatari kwenye kushuka daraja. Pengine ni moja ya vigezo vilivyomfanya kupewa kazi hiyo mpya.
Pengine hataweza kuwapa Kombe la Dunia lijalo ama Euro lakini ataweza kuondoa aibu kwa taifa hilo.
Pia si kukumbana na aibu nyingine waliyopita kwa Iceland.
Kuna wakati kulikuwa na taarifa kwamba kwenye Michuano ya Euro, ndani ya kikosi cha England kulikosekana organisatio, vile vile uhusiano wa kocha na wachezaji haukuwa mzuri na mambo mengine mengi
Allardyce si mtu wa namna hiyo, mara zote timu zake zimekuwa ni zenye mshikamano mzuri na kujituma. Kikubwa kwake huwa ni kufindisha timu za madaraja ya kati.
Wachezaji wengi wa England wamekuwa wakituhumiwa kwa kukosa moyo wa kujituma kwa ajili ya taifa lao, kitu ambacho kwa Big Sam kitakuwa ni mtihani kwake katika kupambana nacho.
Katika maisha yake ukocha Allardyce amewahi kuwa kocha wa Bolton na lakini alishindwa kufanya vyema sana kutokana na ufinyu wa bajeti. Aliwahi kuwafikisha mpaka nusu fainali ya Kombe la FA licha ya kutolewa.
Akiwa West Ham kuanzia mwaka 2011-1025 aliunga-unga na muda mwingi timu hiyo kuwa katika wakati mgumu na kupigania kutoshuka daraja mpaka pale alipotimuliwa.
Mwaka jana pia, pengine ulikuwa mwaka wake wa mafanikio katika maisha yake ya ukocha.
Aliichukua Sunderland ikiwa inataka kuchukua daraja ikiwa nafasi ya 19.
Aliyekuwa kocha wa timu hiyo Dick Advocaat alisema kwamba timu ile haikuwa na kikosi cha ushindani.
Lakini Allardyce aliichukua ile timu na na kufanya mambo makubwa na kuibakisha ligi kuu.
Alisifika kwa kuifanya timu iwe na safu imara ya ulinzi yenye maelewano makubwa na kupandikiza ari ya upambanaji kwa wachezaji, mambo ambayo akiyafanya kwa England yanaweza kuwa msaada kwa timu hiyo akiwa kama kocha.

No comments:

Post a Comment