Sunday, July 24, 2016

Koffi Olomide akamatwa na Polisi Nairobi Kenya


Mwanamuziki wa Congo Koffi Olomide ambaye amewasili Nairobi Kenya asubuhi ya July 22 akiwa na wanamuziki wake pamoja na dancers wake kwa ajili ya show, ameripotiwa kukamatwa baada ya kumpiga teke dancer wake wa kike wakati wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata Nairobi.
Koffi Olomide amekamatwa nje ya studio za Citizen TV usiku huu baada ya video ya tukio la kumpiga dancer wake wa kike kusambaa katika mitandao ya kijamii, hivyo inspector Joseph Boinnet kuagiza askari polisi wamkamate mwanamuziki huyo mkongwe.

No comments:

Post a Comment