Wednesday, October 12, 2016

VPL: Yanga levo kubwa, Simba vinara, Stand united ushindi

VINARA wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Simba Leo wameendelea kujichimbia kileleni baada ya kuifunga Mbeya City wakati Mabingwa Watetezi Yanga wakijikusanya kwa ushindi toka kwa Mtibwa Sugar huku Azam FC wakizidi kudidimia baada ya kufungwa na Stand United iliyojizatiti kushangaza na kuwania Ubingwa.
VPL: LIGI KUU VODACOMMatokeo:Jumatano Oktoba 12Mbeya City 0 Simba 2Mwadui FC 2 African Lyon 0Mbao FC 3 Toto Africans 1Maji Maji FC 0 Kagera Sugar 1Stand United 1 Azam FC 0JKT Ruvu 0 Tanzania Prisons 0Yanga 3 Mtibwa Sugar 1
Jijini Dar es Salaam, Uwanja wa Uhuru, Yanga, waliitwanga Mtibwa Sugar Bao 3-1 walipoongoza 1-0 hadi Haftaimu kwa Bao la Mzambia Obrey Chirwa akifunga Bao lake la kwanza kwenye Ligi ambalo alipachika Dakika 1 kabla Haftaimu.Kipindi cha Pili Mtibwa Sugar walisawazisha Dakika ya 63 kupitia Harun Chanongo lakini Simon Msuva akaipa Yanga Bao la Pili Dakika ya 68 na Mzimbabwe Donald Ngoma, aliengizwa kuchukua nafasi ya Obrey Chirwa aliipa Yanga Bao la 3.Huko Sokoine, Mbeya, Bao za Kipindi cha Kwanza za Ibrahim Ajib na Shiza Kichuya ziliipa Simba ushindi wa 2-0.Nao Azam FC, Timu inayofifia vibaya Msimu huu, ilitunguliwa 1-0 na Stand United, Timu inayokuja juu mno na imo kwenye mbio za Ubingwa, kwenye Mechi iliyochezwa huko Kambarage, Shinyanga.Matokeo haya yamewachimbia Simba kileleni wakiwa na Pointi 20 kwa Mechi 8, wakifuata Stand United wenye Pointi 19 kwa Mechi 9, kisha Kagera Sugar wana Pointi 15 kwa Mechi 9 na Yanga wako Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 14 kwa Mechi 7.Mtibwa Sugar ni wa 5 wakiwa na Pointi14 kwa Mechi 9.----------------------------------------------VPLYANGA - Mechi zao:Okt 16 Yanga v Azam FCOkt 19 Toto African v YangaOkt 22 Kagera Sugar v YangaOkt 26 Yanga v JKT RuvuOkt 29 Yanga v Mbao FCSIMBA - Mechi zao:Okt 15 Simba v Kagera SugarOkt 20 Simba v Mbao FCOkt 23 Simba v Toto AfricanOkt 29 Mwadui v SimbaNov 2 Stand United v Simba----------------------------------------VPL: LIGI KUU VODACOMRatiba:Alhamisi Oktoba 13Ruvu Shooting v Ndanda FC.


Chanzo:Sokaintanzania

PSG wapania kutoa €222 m kuinasa saini ya Neymar Jr

Klabu ya Paris Saint-Germany wameamua kupania kumnasa mshambuliaji wa Brcelona Neymar Jr katika kipindi cha dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiazi.Mabingwa hao wa Ligue 1 wako tayari kuweka mezani dau la euro milioni 222 kwa ajili ya raia huyo wa Brazil kiasi ambacho kitawafanya wampate kutokana na kipengele cha release clause kilichopo kwenye wake na Barcelona (kwa mujibu wa Goal)Goal wameripoti kwamba, vyanzo vya karibu na mchezji vimethibisha kwamba uhamisho huo ulikaribia kukamilika hadi pale Neymar alipoamua kusaini mkataba mpya na Barcelona.PSG wanatarajia kurudi tena kwa mchezaji huyo mara baada ya msimu huu kukamilika.Deal la kumsaijili Neymar litafanikiwa, nyota huyo atashuhudiwa akilipwa mshahara sawa na ule anaolipwa superstar wa Barcelona Lionel Messi.Mkataba mpya wa Neymar unaomalizika 2021 unathamani ya euro milioni 25 kwa mwaka mbali zaidi na ule wa Messi wenye thamani ya euro milioni 42 kama mshahara wake wa mwaka mzima.Endapo Neymar atahamia Paris, ataungana na ndugu zake Marquinhos, Lucas Moura pamoja na Thiago Silva kwenye mji kuu wa Ufaransa.

Baada ya kuchinja kondoo, Iraq yapata ushindi wa kwanza kufuzu Kombe la Dunia 2018

Hii ni katika harakati za kuhakikisha Iraq inafuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 zitakazofanyika Urusi.Hadi sasa Iraq bado hiana ponti katika mchakato wa kuwania kufuzu fainali hizo, tayari imepoteza mechi tatu za kwanza.Ilifungwa 2-0 na Australia, ikapoteza tena na Saudi Arabia 2-1 kabla ya kipigo cha 2-1 kutoka kwa Japan.Tsiku ya Jumanne usiku Iraq ilikuwa inarudi tena uwanjani kupambana na Thailand wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.Katika juhudi zao kubadilisha muelekeao, timu ya taifa ya Iraq ilirudi katika imani za kiroho na kuamua kutoa sadaka ya kondoo kwa kumchinja hadharani wakitaka Mungu awe upande wao kwenye mechi dhidi ya Thailand.Picha ya tukio la kumchinja kondoo hadharani imeenea kwenye mitandao ya kijamii ikionesha namna sadaka ilivyotolewa.Iraqi football fans wait for the start of the 2011 Asian Cup group D football match between Iraq and North Korea at Al-Rayyan Stadium in the Qatari capital Doha on January 19, 2011. AFP PHOTO / ROSLAN RAHMAN (Photo credit should read ROSLAN RAHMAN/AFP/Getty Images)
Mungu amejibu maombi yao, Iraq ikafanikiwa kupata ushindi wao wa kwanza kwenye harakati za kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2018 baada ya kuifunga Thailand kwa magoli 4-0 na kuiacha Thailand ikiburuza mkia kwenye kundi lao ikiwa haina hata pointi moja baada ya kucheza mechi nne na kupoteza michezo yote.


Chanzo: Shaffihdauda

Kwa wanaomsema Zari na Aunt Ezekiel, Wema ana haya!


Mwanadada Wema Isaac Sepetu, amefunguka kuwa anachukizwa na watu wanaomtolea matusi muigizaji mwenzake, Aunt Ezekiel, baada ya kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mzazi mwenza wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

Akizungumza na Za Motomoto News, Wema alisema unatakiwa ufike wakati watu waelewe na waongozwe kwa akili zao za kuzaliwa kwa sababu hakuna kitu kibaya ambacho amekifanya Aunt, kwa kuwa staa mwenzake huyo kwa sasa ni mmoja wa familia hiyo.“Jamani hebu naomba kwanza wamuache Aunt, hana kosa lolote, hata kama ningekuwa mimi hapa nisingeweza kuacha kwenda kwa sababu tayari ni familia na hawezi kumuacha mumewe aende peke yake maana vitu vingine ni vya kujiongeza tu, nachukizwa sana na jinsi wanavyomrushia maneno ya kashfa,” alisema Wema.

New Music Audio: Kcee ft. Tekno – Tender Listen and Download Mp3

Five Star music presents the brand new single from hit-maker KCEE, produced by Mystro and featuring the ‘Pana’ star, Tekno. A mid tempo, hit bound tune entitled ‘Tender.’Enjoy!




Mwalimu aliyemtukana mwanafunzi wa kidato cha sita Iringa, Mahakama imetoa maamuzi!


Ikiwa matukio ya unyanyasaji mashuleni yakiendelea kutokea, Mahakama ya Mwanzo Iringa  Mjini imemuachia huru mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kiwele baada ya kukosa ushahidi wa kumtia hatiani katika kesi ya  kumtukana mwanafunzi.
Mwalimu huyo, Elizabeth Maliga (32) ameshtakiwa kwa madai ya kumtukana mwanafunzi huyo wa kidato cha sita, Rehema Mwakatobe na mama yake.
Amedaiwa kufanya kosa hilo wakati akimsainia Rehema barua ya kumuita mama yake kwenda shuleni hapo kusikiliza kosa la kuchelewa shuleni.
Hukumu hiyo imetolewa wakati Taifa likiwa kwenye mjadala mkubwa baada ya picha za video zilizosambaa mitandaoni kuonyesha kundi la walimu wa Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya likimshambulia mwanafunzi Sestian Chikungu.
Tayari Serikali imeshatangaza kuwafukuza chuo walimu hao na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi.
Akisoma hukumu ya kesi hiyo iliyochukua takriban dakika 45, Hakimu wa Mahakama hiyo,  Abdallah Kutvai alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuishawishi mahakama kumtia hatiani mshtakiwa huyo.
“Jukumu la kuthibitisha kosa ni la upande wa mashtaka. Hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha tano cha Sheria ya Ushahidi ya Mahakama ya Mwanzo iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
“Mashahidi wa upande wa mashtaka wametofuatiana tarehe za kutendwa kosa hilo. Shahidi namba moja ambaye ni mlalamikaji anasema kosa limetendeka Septemba 13, mwaka huu kwenye kikao cha kujadili mwenendo wa utekelezaji wa adhabu zilizotolewa na walimu kwa wanafunzi shuleni hapo,”alisema Hakimu Kutvai.
Amefafanua kuwa shahidi namba mbili alishindwa kubainisha siku ya tukio na kutaja tarehe tatu tofauti, ambazo ni Septemba 13, 14 na 15, siku ambayo mwanafunzi huyo alipewa barua ya kurudishwa nyumbani kwao Dar es Salaam kumfuata mzazi.

Maalim Seif kaandika barua kwenye Benki zote nchini kuzuia Profesa Lipumba kufungua akaunti kwa jina la Chama

Kukiwa bado kuna mkanganyiko wa kisiasa kwenye chama cha CUF sasa Katibu  Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, amemdhibiti mwenyekiti anayetambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba kwa kuandika barua kwa benki zote ili kudhibiti ruzuku ya chama isipite kwenye mikono ya kiongozi huyo.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kumtambulisha Prof. Lipumba Benki ya NMB Tawi la Ilala akitaka apewe ushirikiano wa kufungua akaunti mpya ya chama.

Taarifa kutoka ndani ya CUF zinasema kuwa juzi Maalim Seif, aliandika barua kwa benki zote kuzuia hatua hiyo kwa kuweka zuio la mtu yeyote kufungua akaunti ya chama.

“Unajua hii vita si ya kitoto ni mapambano yaliyopo ndani ya CUF lakini yana nguvu kubwa kutoka katika kila pembe ya watu wanaochukia upinzani. Na pia wapo hata viongozi wakubwa wa dola ambao kila siku wamekuwa wakifanya kazi ya kuivuruga CUF.

“Walitegemea lakini tangu jana (juzi) Katibu Mkuu ameziandikia barua benki zote nchini kuzuia mpango wa Msajili kutaka kuchepusha ruzuku ya chama na kwenda katika mikono ya Lipumba na sasa nakala yake imepelekwa kwa Msajili wa Vyama,” alisema mtoa habari wetu.

Hatua ya Profesa Lipumba kufungua akaunti inatokana na barua aliyopewa na Msajili wa Vyama vya Siasa ya Oktoba 6, mwaka huu iliyosainiwa na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza kwenda kwa Meneja wa Benki NMB Tawi la Ilala.

Katika barua hiyo yenye kumbukumbu namba HA.322/362/14/104  inamtambulisha Profesa Lipumba kutakiwa kufungua akaunti mpya ya The Civic United Front (CUF).

Siri ya Profesa Lipumba kutaka kufungua akaunti mpya yenye jina la Chama cha Wananchi CUF inadaiwa kutolewa na watumishi wa benki wa tawi hilo.

Prof. Lipumba ni Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa, huku chama chake kikiwa tayari kimemfukuza uanachama.

Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kupitia Sisty Nyahoza ilinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari ikikiri kumtambulisha Profesa Lipumba kwa Benki ya NMB ili aweze kufungua akaunti hiyo, hata hivyo ikikana kujua matumizi ya akaunti hiyo.