Showing posts with label Udaku. Show all posts
Showing posts with label Udaku. Show all posts
Wednesday, October 12, 2016
Kwa wanaomsema Zari na Aunt Ezekiel, Wema ana haya!
Mwanadada Wema Isaac Sepetu, amefunguka kuwa anachukizwa na watu wanaomtolea matusi muigizaji mwenzake, Aunt Ezekiel, baada ya kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mzazi mwenza wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Tuesday, October 11, 2016
Lulu anawamwaga wanigeria wakimpasia dili?, Majibu yako hapa.....
Mrembo kutoka Tanzania ambaye ni mwigizaji wa filamu, Elizabeth ‘Lulu ‘ Michael amedai kuwa tangu alipopata tuzo ya AMVCA 2016 amekataa dili kadhaa kutoka kwa wasanii wa muziki wa Nigeria.Muigizaji huyo ameitaja sababu ya kukataa dili hizo imetokana na yeye si mwanamuziki wala video vixen.“Nimepata dili kama mbili tatu kutoka Nigeria za kuigiza filamu na kuna wengine walidhani nafanya muziki,” amekiambia kipindi cha Clouds E cha Clouds TV.“Nimeshatafutwa na wanamuziki wa Nigeria ambao wengine walitaka niimbe na wengine nitokee tu kwenye video zao, siwezi nikawataja,” alisema.March mwaka huu, Single Mtambalike (Rich Rich) na Elizabeth Michael (Lulu) walishinda tuzo za African Magic Viewers’ Choice Awards (AMVCA2016) zilizotolewa nchini Nigeria.
Saturday, October 8, 2016
Amber Lulu ammwagia matusi Giggy Money, Young Dee anahusika!
Baada ya mapema wiki hii kuenea kwa taarifa za kukamatwa kwa model Amber Lulu akiwa na madawa ya kulevya huko mkoani Arusha akijiandaa kwenda nchini China kupitia Nairobi – video vixen hao wameanza kuwashiana moto.
Amber anadaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na rapper Young Dee ameibuka na kuanza kumwagia matusi Giggy Money ambaye aliongea kwenye U-Heard ya Clouds FM na kutoa taarifa hizo za kukamatwa kwake na polisi.
“Muda ambao unahangaika kutafuta kiki ungekuwa unajifunza kuosha k na kutibu hizo fangasi suguu ulizo nazo @gigy_money don’t compare with me iz levels chokoraaaa paka la ambiance stay away from me,” ameandika Amber Lulu kwenye mtandao huo.
Mpaka sasa Giggy hajajibu lolote juu ya ujumbe huo wa matusi aliotumiwa. Amber ameshaonekana kwenye video kadhaa ikiwemo ‘Too Much’ ya Darassa, ‘Inde’ ya Dully Sykes na nyingine.
Friday, October 7, 2016
Video: Mabusu ya Ruby na kijana anayedaiwa kuwa mpenzi wake
Mkali wa wimbo ‘Na Yule’ Ruby ameshare video mbele ya mashabiki wake zaidi ya 260,000 katika mtandao wa instagram akibusiana na kijana anadaiwa kuwa ni mpenzi wake.
Muimbaji huyo alikuwa msiri kwenye mahusiano yake. Wiki hii amepost picha taofauti tofauti za kijana huyo huku akiandika ujumbe wa kimahaba hali ambayo imewafanya mashabiki wake kuhisi huwenda ni mpenzi wake
Katika moja ya picha muimbaji huyo aliandika: Comedian wangu @_mantogoro love you baba nyakunyaku stay away. Katika picha nyingine aliandika “My world” huku akimtag kijana huyo.
Mrembo Amber Lulu Adaiwa Kukamatwa na Madawa ya Kulevya..Marafiki zake Wamkana Live

Mwanadada mrembo ambae amejipatia umaarufu mkubwa siku za karibuni kwa kutokea katika videos kadhaa za Bongo Fleva Amber Lulu inasemekana kwamba yuko chini ya usimamizi wa polisi kwa siku ya pili sasa.
Sababu ya kuwa chini ya Ulinzi inasemekana kuwa amekamatwa na Sembe (Madawa ya kulevya) huko Airport mkoani Arusha akijiandaa kuyasafirisha hadi nchini China.Gossip Cop Soudy brown alizinyaka taarifa hizo na akaona haitakuwa mbaya kama atapiga story na watu wa karibu wa mwanadada Amber Lulu ili kupata ukweli juu ya suala hilo.Ndipo alipomvutia waya Gigy Money. Mapovu yaliyomtoka mwanadada Gigy sio ya polepole, na kudai kuwa kimbelembele cha mwanadada Amber Lulu ndio kimemfanya kupata matatizo.
Soudy Brown hakuishia kwa Gigy tu, alimvutia waya na rapper Young Deeambaye kwa mujibu wa Gigy Money inasemekana kuwa ndiye boyfriend wa mwanadada Amber Lulu. Na Young Dee alikana kabisa kumjua mrembo huyo na akadai kuwa hajui chochote kinachoendelea kuhusiana na msichana huyo.
Kidoa Adai 'Anayenitaka Anifuate na Mabunda Yakutosha'

Mrembo anayepamba video za wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva a.k.a Video Queen, Asha Salum ‘Kidoa’ amefunguka kuwa malipo kidogo anayopata kutokana na kazi hiyo yamemfanya aamue kukaa pembeni na kugeukia uigizaji.
Akizungumza na Gumzo la Town la Mtanzania
Jumamosi, Kidoa amesema kwa sasa yupo bize zaidi katika uigizaji wa tamthilia na filamu mbalimbali.
Anasema: “Hakuna kitu kwenye u-Video Vixen, tunalipwa kidogo sana. Kwa sasa sitaki tena. Naweza kusema hakuna cha maana zaidi ya kuonekana… lakini kama mtu akija na pesa ya maana, naweza kushiriki kwenye video yake.”
Alipoulizwa pesa ya maana ni kiwango gani, haraka alisema: “Pesa ya kueleweka. Nimechoka kufanya kazi isiyokuwa na malengo, mtu akija na milioni yake, naingia mzigoni. Chini ya milioni moja, sishiriki video ya msanii kabisa.”
“Niseme ukweli, kwa sasa najivunia nimekuwa hot cake kwenye tamthilia… natafutwa sana na ninafanya kazi hata tano ilimradi tukubaliane.
“Ujue tamthilia na filamu wananilipa vizuri sana, pesa ambayo sijawahi kulipwa na ninahisi huko kwenye video za wasanii sikuwahi kufikiria kupata fedha kama hizi, ndiyo maana nimefumbuka macho na kuitambua thamani yangu,” anasema.
Anasema pamoja na kwamba kwa sasa amepata
mapokezi mazuri na makubwa kwenye tamthilia na filamu, awali walimgomea wakidhani hana kipaji.
“Mimi kipaji changu hasa ni uigizaji, sikuwa na ndoto za kuwa Video Vixen kabisa. Niliwafuata baadhi ya wasanii na watayarishaji wakubwa lakini walinitosha wakiamini labda sina kipaji, lakini leo hii wameona uwezo wangu wamenikubali.
“Siwezi kukataa kuwa video za wasanii wa
Bongo Fleva zimenisaidia, kwakweli zimenitoa lakini hazilipi. Maisha siyo kuonekana tu, lazima uwe na kitu unaingiza ndiyo utaona raha ya kazi,” anasema Kidoa ambaye video ya Akadumba ya msanii Ney wa Mitego ndiyo iliyomtambulisha.
Chanzo: Mtanzania
“Ujue tamthilia na filamu wananilipa vizuri sana, pesa ambayo sijawahi kulipwa na ninahisi huko kwenye video za wasanii sikuwahi kufikiria kupata fedha kama hizi, ndiyo maana nimefumbuka macho na kuitambua thamani yangu,” anasema.
Anasema pamoja na kwamba kwa sasa amepata
mapokezi mazuri na makubwa kwenye tamthilia na filamu, awali walimgomea wakidhani hana kipaji.
“Mimi kipaji changu hasa ni uigizaji, sikuwa na ndoto za kuwa Video Vixen kabisa. Niliwafuata baadhi ya wasanii na watayarishaji wakubwa lakini walinitosha wakiamini labda sina kipaji, lakini leo hii wameona uwezo wangu wamenikubali.

“Siwezi kukataa kuwa video za wasanii wa
Bongo Fleva zimenisaidia, kwakweli zimenitoa lakini hazilipi. Maisha siyo kuonekana tu, lazima uwe na kitu unaingiza ndiyo utaona raha ya kazi,” anasema Kidoa ambaye video ya Akadumba ya msanii Ney wa Mitego ndiyo iliyomtambulisha.
Chanzo: Mtanzania
Thursday, July 28, 2016
Aunt Ezekiel Akimbilia Gym Kuokoa Penzi Lake
Staa wa filamu, Aunt Ezekiel aliye katika mapenzi na Dansa Moses Iyobo, ameamua kukimbilia gym kwa ajili ya kupunguza unene unaomuandama ili kulinusuru penzi lake.
Akizungumza na Za Motomoto News, Aunt amesema ameanza mazoezi ya nguvu kila asubuhi ili aweze kupunguza mwili aendane na mpenzi wake kwani mwili wake ni mkubwa kuliko wa mwenzie.
“Daah, nimeona nitapoteza penzi langu bure, nimekuwa mnene kumpita baby kitu ambacho siyo sawa, nilikuwa na kilo 87, hivi sasa nimepunguza kilo sita,” alisema.
Kajala Masanja amlilia Mume wake Gerezani
Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ hivi karibuni amekwenda kumlilia mumewe, Faraji Chambo anayetumikia kifungo cha miaka kumi na mbili gerezani.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Kajala, mwanamama huyo alitinga kwenye Gereza la Ukonga, Dar alikofungwa mumewe ambapo alipata nafasi ya kumjulia hali kisha kumwaga machozi akimuonea huruma anavyosota gerezani hasa akikumbuka walivyokuwa wakiishi kabla ya msala huo.
Katika safari hiyo, Kajala aliongozana na mwanaye, Paula Paul na mdogo wake Kajala ambao ndiyo waliokuwa wakimtuliza staa huyo ambaye alisababisha mumewe naye kutokwa machozi.
Akizungumzia ishu hiyo, Kajala ambaye wiki iliyopita alizindua filamu yake kali ya Sikitu alisema kuwa ni utaratibu wake wa mara kwa mara kwenda kumjulia hali mumewe huyo ila mara zote huwa anakwenda kimyakimya.
“Huwa nakwenda mara nyingi tu sema ndiyo hivyo huwa sipendi kuongozana na msururu mrefu, namshukuru Mungu anaendelea vizuri,” alisema Kajala. Machi 2013, Kajala na Faraji walihukumiwa ambapo Kajala alitakiwa kwenda jela miaka mitano au faini ya shilingi milioni kumi na tatu na mumewe miaka kumi na mbili au faini ya shilingi milioni mia mbili kwa kosa la kutakatisha fedha haramu kwenye Benki ya NBC, Tawi la Dar.
Hata hivyo, Faraji alishindwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kujikuta ‘akiozea’ gerezani huku Wema Sepetu ‘Madam’ akimlipia Kajala faini ya shilingi milioni kumi na tatu, iliyomnusuru kwenda jela.
Subscribe to:
Posts (Atom)




