Friday, July 29, 2016

Kampuni ya Apple Music imekuwa ya kwanza kufanya mauzo ya albam mpya ya Dj Khaled

Tayari albamu mpya ya Dj Khaled inayokwenda kwa jina la ‘Major Key’ imeanza kupatikana kwenye mtandao wa Apple Music
Khaled ameachia albamu hiyo yenye nyimbo 14 akiwa chini ya menejimenti yake mpya ya Roc Nation inayomilikiwa na rapper Jay Z, kupitia akaunti yake ya twitter ameandika, “#Major officially on iTunes now !!! FANLUV!!! Let’s go!!!!!!.”
Hizi ni nyimbo zilizopo kwenye albamu hiyo:
1. “I Got the Keys” (feat. JAY Z & Future)
2. “For Free” (feat. Drake)
3. “Nas Album Done” (feat. Nas)
4. “Holy Key” (feat. Big Sean, Kendrick Lamar & Betty Wright)
5. “Jermaine’s Interlude” (feat. J. Cole)
6. “Ima Be Alright” (feat. Bryson Tiller & Future)
7. “Do You Mind” (feat. Nicki Minaj, Chris Brown, August Alsina, Jeremih, Future & Rick Ross)
8. “Pick These Hoes Apart” (feat. Kodak Black, Jeezy & French Montana)
9. “F**k Up the Club” (feat. Future, Rick Ross, YG & Yo Gotti)
10. “Work for It” (feat. Big Sean, Gucci Mane & 2 Chainz)
11. “Don’t Ever Play Yourself” (feat. Jadakiss, Fabolous, Fat Joe, Busta Rhymes & Kent Jones)
12. “Tourist” (feat. Travis Scott & Lil Wayne)
13. “Forgive Me Father” (feat. Meghan Trainor, Wiz Khalifa & Wale)
14. “Progress” – Mavado

Tayari ratiba ya treni mpya Dar imetoka jijini Dar es Salaam


Uongozi wa kampuni ya reli Tanzania ‘TRL’ umetangaza kubadilishwa kwa muda wa kuondoka treni ya abiria kutoka Dar es salaam kwenda bara kuanzia August 02 2016, ambapo treni itaondoka saa 9 alasiri badala ya saa 11 jioni ilivyozoeleka.
Mabadiliko hayo yamefanyika ili kutoa nafasi kwa treni ya pili ya huduma ya jiji kutoka kituo kikuu cha reli cha Dar es salaam kwenda Pugu ambayo itaanza kutoa huduma Jumatatu Agosti Mosi, 2016.
Aidha huduma mpya ya treni ya jiji kwenda Pugu itakuwa na vituo 10 kama ifuatavyo,Pugu stesheni, mwisho walami, Gongo la mboto, FFU Mombasa, Banana njia panda kwenda Segerea) na Karakata, vingine ni pamoja na Vingunguti Mbuzi, SS Bakhressa, kamata na kituo kikuu cha reli Dar es salaam.
Huduma ya treni imeelezwa itakuwa ya awamu mbili asubuhi na alasiri ambapo treni ya kwanza itaondoka kituo cha Pugu saa 12 asubuhi na kuwasili kituo cha Dar es salaamsaa 12:55 asubuhi na kufanya safari 3 zitakazomalizika saa 05:15 asubuhi.
Jioni pia kutakuwa na safari 3 ambapo treni ya kwanza itaondoka kituo cha Dar es salaamsaa 09:55 alasiri kwenda pugu na kuwasili saa 10:50 jioni na safari ya mwisho kutoka Pugu kwenda Dar es salaam itakuwa saa 03:20 usiku.

New Music Videi: Nikki wa Pili ft ChinBeez - Sweety Mangi | Watch and Download Free


Itizame nyimbo mpya ya Nikki wa pili kutoka kampuni ya Weusi inaitwa Sweety Mangi ambayo amemshirikisha Chin Beez kisha uache maoni yako.

Justin Campos kutoka Afrika kusini ndiye kaitayarisha.

DC MTATURU AZINDUA UCHANGIAJI WA DAMU SALAMA, MFUKO WA AFYA (CHF) NA DAFTARI LA UFUATILIAJI


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akichangia damu kwa ajili ya wananchi wanaofariki kwa kukosa huduma ya damu katika hospitali mbalimbali nchini


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akihojiwa kuhusu umri na mambo kadha wa kadha ili kufanyika utambuzi kama damu yake inatosha kiasi cha kutoa kwa ajili ya wengine, Mtaturu amechangia Unit 450 ya damu yaani chupa moja.


Na Mathias Canal, Singida

Wananchi wametakiwa kufanya kazi kwa kushiriana na viongozi na watumishi wengine wa afya ili kuleta mabadiliko na kuhakikisha kuwa maisha ya wananchi yanakuwa bora zaidi.


Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Jumanne Mtaturuwakati wa uzinduzi wa uchangiaji wa damu salama, Mfuko wa Afya (CHF) na Daftari la ufuatiliaji akinamama wajawazito Wilayani humo.


Akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo Mtaturu amesema kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali  suala la vifo vya kina mama wajawazito, watoto wadogo pamoja na upungufu wa dawa katika vituo vya afya bado ni changamoto.


Amesema Takwimu zinaonyesha kuwa katika Wilaya ya Ikungi vifo vya akina mama vinaongezeka mwaka hadi mwaka ikiwa mwaka 2013 ilikadiriwa kupoteza akinamama 79 kwa kila vizazi hai 100,000 na hesabu hiyo imeongezeka na kufikia 94/100,000 kwa mwaka 2014 na 201/100,000 kwa mwaka 2015.

“Hali hii haikubaliki ndugu zangu wa Kata ya Minyughe na Wilaya ya Ikungi kwa ujumla  mbaya zaidi matatizo yanayopelekea vifo hivyo yanatokana na sababu ambazo zinaweza kuzuilika, kwa mfano, ukosefu wa damu katika vituo vyetu vya afya na kutozingatia vidokezo vya hatari tunavyoelekezwa wakati wa mahudhurio ya kliniki” Alisema Mtaturu.


Sanjari na hayo Mtaturu alisema kuwa  matatizo makubwa yanayopelekea vifo vya akina mama wajawazito ni kutokuzingatia vidokezo hatari kama wataalamu wanavyoelekeza  kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, hali ambayo inapelekea akinamama wanaotakiwa kujifungua Hospitalini wanalazimika kujifungulia nyumbani au kwenye Zahanati ambapo pakitokea dharura wanashidwa kupata msaada.


Kutokana na hali hiyo Mtaturu amesema kuwa ili kuhakikisha wajawazito wote wanaenda Kliniki na kufuata wanayoelekezwa Wilaya ya Ikungi imeanzisha daftari la ufuatiliaji ambapo jamii itasaidia kuwakumbusha wajawazito kwenda Kliniki na kuchukua hatua pale ambapo hawatafanya hivyo.


“Lengo kuu ni kuhakikisha akina mama wajawazito wote wanahudhuria kliniki mapema  na kuhudhuria angalau mara nne ili kupunguza vifo ambavyo vinaweza kuzuilika Sasa ninawataka wenyeviti  na watendaji wote wa vijiji kufanya ufuatiliaji wa daftari hilo kuona kama akina mama wajawazito  wanahudhuria kama wanavyotakiwa na kunipatia taarifa ya utekelezaji wake kila mwezi.”Alisema Mtaturu

Akizungumzia suala la ukosefu wa damu salama katika vituo vya afya Mtaturu amesema kuwa Wilaya ina mahitaji ya wastani wa Unit 1000  kwa Mwaka na kwa kuzingatia hilo umewekwa  mkakati wa kuhamasisha jamii angalau iweze kutoa damu mara moja kila mwezi kwa kila Kata.
“Kwa Mwananchi au mtu yeyote ambaye atakuwa amepata tatizo la upungufu wa damu na kuhitaji kuongezewa damu katika hospitali zetu hatahitajika kulipia gharama yeyote inayohusu kuongezewa damu kwa sababu tutakuwa tumejiwekea akiba ya damu yetu wenyewe” Alisema Mtaturu.

Aidha Mtaturu ameongeza kuwa  mabadiliko katika sekta ya Afya yanayoendelea kutekelezwa katika utoaji huduma yana lengo la kuinua kiwango cha ubora wa huduma za afya kwa wananchi na kuongeza kiwango cha uwajibikaji kwa wasimamizi na watoaji wa huduma hizo na ili kufanikisha lengo hilo, madaraka, majukumu na kazi, rasilimali zaidi za Afya zinahitajika kwa kuitaka jamii kuchangia katika mifuko ya afya ya jamii (CHF).


Alisema Mfuko wa afya ya jamii (CHF) kwa Kaya moja itatakiwa kuchangia Tsh. 10,000/= na atatibiwa Baba, Mama na Watoto wanne kwa mwaka mzima na kuongeza kuwa mfuko huo hautaimarika kama hautakuwepo usimamizi imara na unaoambatana na uadilifu.

“Miongoni mwa manufaa ya mabadiliko ya sekta ya afya ni pamoja na jamii yenyewe kuwa na madaraka zaidi ya kuamua kuhusu huduma za afya zinazotolewa na kushiriki kikamilifu katika utoaji wa huduma hizo kwa kuwakilishwa katika bodi ya afya ya wilaya na kamati za huduma za afya za vituo” Alisema Mtaturu


Katika kuhitimisha uzinduzi huo Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi Mtaturu Jumanne Mtaturu alizindua rasmi matumizi ya Daftari la ufuatiliaji kwa kuwakabidhi madaftari hayo wenyeviti wa vitongoji wa kata hiyo pamoja na kuanza zoezi la utoaji damu kwa wilaya nzima ya Ikungi.

Jumla ya Watu waliochangia Damu ni 36 ambapo Wastani wa damu iliyotolewa kwa mtu mmoja ni Unit 450. Hivyo tukizidisha 36 × 450 tunapata Unit 16,200 ambazo ni sawa na lita 16.2 za Damu zilizopatikana mara baada ya uzinduzi.

DC Mtaturu amehamasisha wananchi Wilayani Ikungi kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii (CHF) kwani itasaidia kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa Wilaya ya Ikungi ambayo ina Kaya 53823 huku wananchi waliojiunga na mfuko huo wakiwa ni asilimia 24% tu.

Thursday, July 28, 2016

Aunt Ezekiel Akimbilia Gym Kuokoa Penzi Lake



Staa wa filamu, Aunt Ezekiel aliye katika mapenzi na Dansa Moses Iyobo, ameamua kukimbilia gym kwa ajili ya kupunguza unene unaomuandama ili kulinusuru penzi lake.

Akizungumza na Za Motomoto News, Aunt amesema ameanza mazoezi ya nguvu kila asubuhi ili aweze kupunguza mwili aendane na mpenzi wake kwani mwili wake ni mkubwa kuliko wa mwenzie.

“Daah, nimeona nitapoteza penzi langu bure, nimekuwa mnene kumpita baby kitu ambacho siyo sawa, nilikuwa na kilo 87, hivi sasa nimepunguza kilo sita,” alisema.

Mrembo Tunda Afunguka Kumwagana na Mwanamuziki Young D



Mrembo mwenye umri mdogo muuza sura Bongo, Tunda Sebastian amefunguka kumwagana na mwandani wake wa muda mrefu, ambaye ni staa wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young D’ na kusema ameamua kujiweka kando kwenye maswala ya mapenzi.

Akipiga stori na Showbiz Xtra baada ya kumbananisha kuhusiana na tetesi za uhusiano wake kuvunjika kutokana Young D kubaini anatoka na mwanamuziki mwenziye (jina kapuni) ndipo akaeleza kuwa, ishu hiyo haina ukweli ila ameachana na mwandani wake huyo kwa sababu ambazo hawezi kuzianika kwa sasa.

“Hayo ya kutoka na huyo msanii si kweli na kuhusu Young D nimeshaachana, sifikirii kuwa na msanii yeyote na sihitaji mpenzi kwa sasa,” alisema.

Kajala Masanja amlilia Mume wake Gerezani


Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ hivi karibuni amekwenda kumlilia mumewe, Faraji Chambo anayetumikia kifungo cha miaka kumi na mbili gerezani.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Kajala, mwanamama huyo alitinga kwenye Gereza la Ukonga, Dar alikofungwa mumewe ambapo alipata nafasi ya kumjulia hali kisha kumwaga machozi akimuonea huruma anavyosota gerezani hasa akikumbuka walivyokuwa wakiishi kabla ya msala huo.
Katika safari hiyo, Kajala aliongozana na mwanaye, Paula Paul na mdogo wake Kajala ambao ndiyo waliokuwa wakimtuliza staa huyo ambaye alisababisha mumewe naye kutokwa machozi.
Akizungumzia ishu hiyo, Kajala ambaye wiki iliyopita alizindua filamu yake kali ya Sikitu alisema kuwa ni utaratibu wake wa mara kwa mara kwenda kumjulia hali mumewe huyo ila mara zote huwa anakwenda kimyakimya.
“Huwa nakwenda mara nyingi tu sema ndiyo hivyo huwa sipendi kuongozana na msururu mrefu, namshukuru Mungu anaendelea vizuri,” alisema Kajala. Machi 2013, Kajala na Faraji walihukumiwa ambapo Kajala alitakiwa kwenda jela miaka mitano au faini ya shilingi milioni kumi na tatu na mumewe miaka kumi na mbili au faini ya shilingi milioni mia mbili kwa kosa la kutakatisha fedha haramu kwenye Benki ya NBC, Tawi la Dar.
KajalacropHarusi
Hata hivyo, Faraji alishindwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kujikuta ‘akiozea’ gerezani huku Wema Sepetu ‘Madam’ akimlipia Kajala faini ya shilingi milioni kumi na tatu, iliyomnusuru kwenda jela.