Saturday, May 21, 2016

Wewe sio mwaminifu kwa mpenzi wako?, umejiuliza kwanini....!!!?


Hapa nazungumza na wale ambao wanatamani kuwa waaminifu kwa wapenzi wao. Yapo mambo mengi, lakini hapa ninajitahidi kueleza yale ya muhimu zaidi. Wiki iliyopita niliishia kwenye kipengele cha mitandao ya kijamii, kwa kuwa sikukimaliza, tutaendelea hapo.MITANDAO YA KIJAMII
Utafiti usio rasmi unaonesha kwamba, pamoja na kwamba mitandao ya kijamii imesaidia kwa kiasi kikubwa sana kurahisisha upatikanaji wa taarifa, kuendesha mijadala na kukuza ufahamu wa mambo mengi, suala la mapenzi limetajwa!

Utakutana na mtu Facebook (mfano), mmekuwa marafiki, lakini siku ya siku anaanzisha mambo ya mapenzi. Kwa sababu umeshakuwa naye karibu kwa muda mrefu, umekuwa wazi kwake ni rahisi kuanguka!
Hisia za mapenzi wakati mwingine hudanganya. Ngoja niwaambie ukweli, unapokuwa unawasiliana sana na mtu wa jinsi tofauti na yako, hisia za mapenzi huwa kali sana, kiasi kwamba ukiambiwa tu unapendwa, ni rahisi kuingia mkenge!

Kwenye mitandao ya kijamii kwa mfano Facebook, BBM, Twitter na mingineyo maarufu kuna utamaduni wa kuweka picha. Wakati mwingine picha hudanganya...kwa haraka haraka mtu eti anasema amekupenda. Hakuna lolote zaidi ya kuwaza ngono tu!
Huo ndiyo ukweli. Tatizo ni kwamba, huwezi kujua kama kuna hatari hiyo mbele yako. Unao marafiki wengi, mnataniana kila wakati, siku akilianzisha, inakuwa ngumu kuchomoka. Hata hivyo, kuna mambo madogo sana ukiyafanya yatasaidia kukutoa kwenye mtego.
Utakuta mtu ana mpenzi wake, mke au mume. Kifupi yupo kwenye uhusiano, lakini kwenye mtandao anaandika yupo ‘single’. Kwa nini hutaki kujulikana kuwa upo kwenye uhusiano?
Hujiamini? Humpendi mpenzi wako au tatizo ni nini hasa? Rafiki zako wanapoona huna mtu kwenye maelezo yako, wanatumia nafasi hiyo kukutega. Kwa nini ujiweke kwenye mitego? Kama upo kwenye uhusiano, kuwa mkweli, andika.
Ikiwezekana sehemu ya kuweka picha yako, weka ya mpenzi wako au mliyopiga pamoja, hii itasaidia marafiki kukuheshimu na wale wenye tabia za kipuuzi kujitoa mapema.
Wanaotumia mitandao ya kijamii ni mashahidi wa hiki ninachokizungumzia hapa.

MAVAZI
Kipengele hiki kinawagusa zaidi wanawake. Mavazi yanazungumza! Ulivyovaa ndivyo unavyojitafsirisha kwa wanaokutazama. Inawezekana ukawa ni mwaminifu kwa mwenzako na unajitahidi sana kuhakikisha unakuwa katika hali hiyo, lakini mavazi yako yanaweza kukutibulia.

Kwa nini uvae nguo zinazoonesha maungo yako ya ndani? Mchumba au mke wa mtu, kwa nini uvae vinguo vya ovyo? Unamwonesha nani sasa huko barabarani? Ndugu zangu, sijawahi kuona mwanamke aliyevaa kiheshima akapata usumbufu kwa wanaume njiani.
Hata kama unajijua huwezi kutegeka, lakini nataka kukuhakikishia kwamba, kusumbuliwa sana ni njia ya kuelekea kwenye usaliti. Ipo mifano hai; Kuna dada mmoja alikuwa anavaa vinguo vya kubana, kila akipita anasumbuliwa na mwanaume fulani hivi mtaani kwao.

Ameshamtumia watu mara nyingi, lakini anakataa. Siku moja ikatokea amehitilafiana na mpenzi wake, kwa hasira akaamini kuwa ameshaachana naye na hamtaki tena. Alipopita ile sehemu, yule jamaa akamuita.
Akilini mwake, akaona hakuna sababu ya kumtesa yule jamaa wakati amegombana na mpenzi wake. Kwa lengo la kujiliwaza akaenda, jamaa alilala naye siku hiyo hiyo! Alijuta baada ya kumaliza tendo!
Ya nini yote hayo? Vaa mavazi ya heshima. Jisogeze kwenye uaminifu. Ni nani atakayekusumbua ikiwa mavazi yako yanaonesha heshima uliyonayo?
Usikose wiki ijayo katika sehemu ya mwisho, kuna mambo mengi ya muhimu unayotakiwa kujua.

Friday, May 20, 2016

NEW MUSIC VIDEO: Shilole ft Barnaba - Say my name ( Watch Official Video )

Shilole a.k.a Shishi Baby kwa kushirikiana na Barnaba wanatualika kutazama video yao mpya ‘Say My Name’ na ukishaitazama uiache comment yako....

Friday, April 22, 2016

NEW MUSIC VIDEO - Galatone - Samaki


Karibu kutizama video mpya ya Galatone inayokwenda kwa jina la Samaki ambayo audio yake imekua inaingizwa kwenye playlist za vituo mbali mbali vya
redio nchini.

Tizama kisha uache maoni yako hapo chini.

NEW MUSIC VIDEO AND AUDIO: Tay Grin ft 2Face Idibia - Chipapa


Msanii kutoka Malawi Tay Grin wamejuana muda mrefu n msanii wa Nigeria 2face Idibia.  “Nimemfahamu 2 Baba kwa miaka mingi na tumekuwa tukiongea siku zote kuhusu kola
bo. Ni msanii 

mwenye kipaji kikubwa na kufanya kazi naye ni furaha kubwa 

kwangu,” anasema Tay.
Akiutambulisha Chipapapa kwa wapenzi wa muziki Afrika Mashariki, Tay ametoa ujumbe huu kwao: Nikijitambulisha tena kwa Afrika Mashariki, ningependa kuwashukuru mashabiki wangu wa kitambo kwa kuniunga mkono pamoja na muziki wangu. Kwa mashabiki wangu wapya, salamu za pekee kutoka Malawi kwenu nyote. Nina hamu kubwa ya kuja kwenu na kuwaburudisha.”
Video ya Chipapapa ilifanyika Afrika Kusini kwenye mji wa machimbo ya madini wa Nigel na kuongozwa na Bruce Patterson. Ni video inayoonesha uzuri wa Afrika kwa kutumia uchezaji, rangi na watu wazuri waliovaa nguo mbalimbali za Kiafrika.

Thursday, April 21, 2016

NEW MUSIC AUDIO

Chris Brown - Shut down Mp3
Msanii kutoka Marekani Chris Brown ambaye ni msanii mwenye jina kubwa hususan kwenyemuziki wake anaoufanya yaani RnB ameachia wimbo wake huu mwingine uitwao
Shut down.

Karbu kuusikiliza kisha uache maoni yako hapo chini.


Wednesday, April 20, 2016

NEW MUSIC AUDIO: Nasi ft Shaa - Nikilewa


Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutokea hapa mkoani Iringa ambaye pia ni Dj na mtangazaji wa redio Ebony Fm ameachia audio ya wimbo wake mpya uitwao Nikilewa ambao
amemshirikisha Shaa Producer akiwa ni Daxochalli.

Sikiliza na kudownload hapa chini:-


NEW MUSIC VIDEO: Nasi ft Shaa - Nikiliewa


Huyu jamaa ni Dj wa kituo cha redio Ebony fm Iringa ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao nikilewa ambao amemshirikisha
Shaa.

Director ni Deo Abel. Itizame hapa chini.