Inatokea kwenye gereza la Naivasha Kenya ambapo Mfungwa Michael Kahiga ni miongoni mwa Wafungwa wachache watakaojiunga na chuo kikuu kutokana na jitihada zake za kujisomea kwa bidii chini ya Mwalimu wake pia ambaye pia ni Mfungwa wa kifungo cha maisha.
Kwenye gereza hilo la Naivasha kuna Liblary ambayo ina vitabu mbalimbali ambapo Michael anasema pamoja na yeye kufaulu kwenda chuo kikuu, kwenye kusoma kwake akiwa gerezani bado hakuwa na Waalimu ambao wamekidhi vigezo.
Michael anatumikia kifungo cha miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya wizi ambapo baada ya kumaliza kifungo chake, atajiunga na chuo kikuu cha London Uingereza ambacho kimempa nafasi ya kusoma bure kwenye chuo hicho baada ya kufaulu vizuri kwenye mtihani wa kitaifa gerezani.
Kwa mujibu wa K 24 Kenya, kwenye mtihani aliofaulu Michael ni Wanafunzi 141 walipata A ambapo Michael mwenyewe alipata C+, unaweza kumtazama kwenye hii video hapa chini.