Friday, January 27, 2017

Madee Azungumza Kuhusu Babu Tale Kujitenga na TipTop, Fahamu Kuhusu Diamond Platnumz Kuhusuka Nao


Msanii anayefanya vizuri na ngoma inayokwenda kwa jina Hela, Madee amesema kuwa hajui lolote kuhusu wanaosema kuwa Meneja wa Tip Top "Babu Tale" amekuwa akiegemea sana katika kusapoti mziki wa WCB na kuwasahau kina Tunda, yeye mwenyewe Madee na Dogo Janja.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio Madee amesema kuwa kwa sasa anaangalia zaidi muziki wake na wa dogo Janja, na kwamba kundi la TipTop bado lipo na kuna mambo mengi ambayo yanakuja katika kundi hilo.

Aidha Madee alipoulizwa kuhusu ujio wa ngoma ya wasanii wote wa TipTop ameeleza kuwa ipo ngoma waliyoifanya na Diamond Platnumz ambayo bado hawajaiachia mpaka ngoma za kila mmoja kufanya vizuri ndipo wataangalia kama kuna uwezekano wa kuiachia.


No comments:

Post a Comment